BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA UBUNGO LAANZA KAZI BAADA YA MADIWANI KUAPA NA KUCHAGUA MEYA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha Katikati ,aliye upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Manispaaya ya Ubungo Beatrice Dominic na aliye upande wa kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori wakiwa mbele ya mkutano wa Baraza kwa Mara ya kwanza baada ya Madiwani kuapishwa .(Picha na John Luhende)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha Katikati ,aliye upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Manispaaya ya Ubungo Beatrice Dominic na aliye upande wa kushoto ni Naibu Meya wa Manispaaya Ubungo Hassan Siraji Mwasha, wakiwa mbele ya mkutano wa Baraza kwa Mara ya kwanza baada ya Madiwani kuapishwa .(Picha na John Luhende)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha ,aliye upande wa kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Hassan Siraji Mwasha, Wakiwa tayari kuendesha kikao Cha Baraza la Madiwani baada ya kuchaguliwa.
Na John Luhende
Msimamizi wa uchaguzi wa Meya Manispaa ya Ubungo Ndugu James Mkumbo ambaye ni katibu tawala wa Wilaya ya Ubungo amemtangaza Jaffary Juma Nyaigesha, Diwani wa kata ya Ubungo kuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo.
Nyaigesha amechukua nafasi hiyo baadaya ya kupata kura zote 22 kati ya kura zilizopigwa ,huku Hassan Siraji Mwasha Diwani wa kata ya Msigani, akichaguliwa kuwa Naibu Meya baada ya kupata kura .
Nyaigesha akizungumza wakati akijinadi kuomba kura amesema kabla ya kuomba nafasi ya Meya alipitia nafasi mbali mbali ikiwemo Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa akiwa mwenyekiti wa wenye Viti Wilaya ya Kinondoni kabla ya kutengwa kwa Ubungo kuwa Wilaya na kueleza kuwa anaouzoefu na baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani amepita maeneo mbalimbali hivyo anazifahamu changamoto za Manispaa hiyo .
Kwa upande wake Naibu Meya akitoa shukrani baada ya kuchaguliwa amewataka Madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano huku akiahidi kuwapa ushirikiano na ktofanya upendeleo wa ainayoyote.
Awali kabla ya uchaguzi huo Madiwani wateule wa Manispaa ya Ubungo leo wamekula kiapo rasmi kwa kuanza kutekeleza majukumu yao ya uwakilishi wa wananchi Katika Manispaa na utekelezaji wa shuguli za Maendeleo.




Post a Comment