Ads

KANISA HALISI LA MUNGU BABA, WAZINDUA KITABU CHA UFAHAMU ULIO ANZIA TANZANIA KWENDA KWA MATAIFA ,MAKUHANI WASHUHUDIA MAZITO KUHUSU TANZANIA.

 



Na John Luhende

Makuhani  wa kanisa la halisi la Mungu Baba , wame shuhudia  jinsi ambavyo Tanzania,ilivyo barikiwa na Mungu Baba  ambapo wamekiri kuwa Taifa la Tanzinia Mungu amelipa kibali mbele ya mataifa na kwamba baraka zianaanzia hapa.

Awali kiongozi wa kanisa hilo  Baba wa Uzao alimesema, kutokana na upendeleo huo wa Mungu Baba kwa Tanzania ndiyo sababu Mataifa mengi Duniani sasa yanaitazama nchi Tanzania kwa namna ya kustaajabishwa kiasi kwamba wengine kuamua kuja, ili kushuhudia ufahamu huu ulioanzia katika taifa hili.
Hata hiyo Baba wa uzao akizindua kitabu hicho amesema kuwa uzinduzi huu, siyo kwa ajili ya kushindana na yeyote, wala siyo tamasha, au 'Crusade' au Kanisa hilo  kujimwambafai   bali kuna mambo makuu manne ambayo watanzania wayajue, ikiwemo kuwafahamisha kuwa neema hii inayoipata Tanzania hadi kuvuma duniani katika kufanikiwa kwenye mambo mengi ikiwemo kundokana na janga la Corona ambalo bado linayasumbua mataifa mengi, ni kwa sababu Mungu Baba amelipa Taifa hili upendeleo wa makusudi.
Uzinduzi wa Kitabu cha  'ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda katika mataifa mengine' ili kusikia na kuupokea upendeleo ambao Mungu Baba ameipa Tanzania na kung'ara katika kila jambo ikiwemo kuwa na amani, utulivu na uchumi wake kukua kwa kasi ya kushangaza umefanyika leo jumapili katika uwanja wa uhuru Temeke Jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na maelfu ya watu walioalikwa kutoka mikoa mbalimbali na kutoka nchi zaidi ya sita, ikiwemo Congo DRC, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Msumbiji ambapo makuhani kutoka nchi zizo wameshuhudia mabo mbalimbali ambayo Nchi ya Tanzania imebarikiwa 

Kuhuni kutoka Mombasa kenya akishuhudia mbele ya mkutano  amesema,  waandishi wa habari nchini Kenya baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT John Pombe Magufuli  kutangaza kuwa watanzania hawatavaa barakoa walisema Kama Kuna Rais ataaaibika ni huyo .

Lakini baada ya kuona hali inazidi kuwa nzuri walibaki bila kujua nini kimetokea, lakini amesema Kama kuna mtu anataka kuona watu wanavyo hangaika  na CORONA avuke mpaka aende Kenya.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Kuhuni kutoka Zambia ambapo naye alisema  hakuna Rais Katika Dunia aliye waambia wananchi wake kuwa "Watanzania  msiogope ,Corona ni mafuatu ya kawaidatu  yatapita "amesema Kuhani huyuo.

Amesema Tanzania Mungu ameiinua kutoka mataifa kwamaana hata katikati ya ugonjwa wa CORONA imetangazwa kuwa Nchi ya uchumi wakati ,na kuongeza kuwa sauti ya Mungu Baba iko ndani ya Taifa hili.

Kwa upande wake Kuhani kutoka Uganda , amewataka watanzania kujitambua kuwa wao ni chanzo Cha baraka,nataifa hili Mungu alilianda tangu mwanzo .

"kwavurugu tulizokuwanazo  Uganda miaka ya utawala wa Idiamini  Dada majeshi ya Tanzania ndiyo yalikuja kuwa kutukomboa waganda ,niliamua kujitangaza kuwa na Mimi ni mtanzania  kwa hiari , askari wa Uganda walikuwa wamezoea kuwanyanyasa watu"Amesema 

Wanajeshi wa Tanzania japo walikuwa Katika hali ya Vita walikuwa na upendo wa ukombozi ,watanzania wliikomboa Uganda na  wamekomboa nchi nyingi na sasa Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji mkutano  wa nchi Duniani zitakazo jadili amani.

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Watanzania wote bila kubagua dini au itikadi za kisiasa wamefika  kwa wingi kwenye uzinduzi wa Kitabu hicho.


No comments