Ads

MADIWANI WA MANISPAA YA ILALA WAAPISHWA, OMARY KUMBILAMOTO RASMI MSTAHIKI MEYA ILALA

 Diwani wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Omary Kumbilamoto akiapishwa leo jijini Dar es Salaam.

Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo wamempitisha Diwani wa Kata ya Vingungiti Omary Kumbilamoto kwa Mstahiki Meya wa manispaa hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kupita bila kupingwa, Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe. Omary Kumbilamoto, amesema kuwa umoja na ushirikiano ni nguzo muhimu katika kuhakikisha Manispaa inapiga hatua katika nyanya mbalimbali za kimaendeleo. 

Mhe. Kumbilamoto amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na madiwani kwa kumuamini kumchangua tena kuwa Mstahiki meya, huku akiwahidi kuwaunganisha madiwani wote kuwa kitu kimoja. 

"Nitahakikisha tunatekeleza ilani ya Chama cha CCM pamoja miradi mbalimbali ambayo serikali kwa ujumla imekusudia kutekeleza katika Manispaa ya Ilala" amesema Mhe. Kumbilamoto.

Amebainisha kuwa asilimia kubwa madiwani wengi  katika uchaguzi mkuu mwaka huu, wamechanguliwa na wananchi kwa kusafiria nyoto ya Rais Dkt. Magufuli kutokana na kazi kubwa aliyoifanya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Ili mabara hilo kufikia lengo, Mhe. Kumbilamoto amewataka madiwani wote kumtegemea Mungu katika utekelezaji wa majukumu kutokana yeye ndiyo msaada kwa kila jambo. 

Katika hatua nyengine madiwani wote wa Manispaa ya Ilala waliapishwa kwa ajili kuanza majukumu yao kuwatumikia wananchi.


No comments