Ads

WAZIRI JAFO ARIDHISHWA NA KASI NA UBORA UJENZI NYUMBA ZA WATUMISHI KIGAMBONI

 

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Serikali za Mitaa na Tawala za mikoa Mhe.Suleiman Jafo aliye vaa koti jeusi akiwaelekeza jambo viongozi wa Manispaa ya Kigamboni  wakwanza upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale anaye fuata upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya Mhe.Sara Msafiri  akifuatiwa na katibu tawala  wilaya hiyo Dalmia Mikaya(Picha na John Luhende)
Moja ya nyumba zinazo jengwa kwaajili ya watumishi wa Manispaa ya Kigamboni
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Serikali za Mitaa na Tawala za mikoa Mhe.Suleiman Jafo  aliye katikati   akielekea kufanyaukaguzi wa nyumba za watumishi wakwanza upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale anaye fuata upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya Mhe.Sara Msafiri , wakwanza kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Ernest  Mafimbo akifutiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dr es salaam Aboubakar Kunenge.

Na John Luhende

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Serikali za Mitaa na Tawala za mikoa Mhe.Suleiman Jafo , ameiagiza Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha nyumba za watumishi zimekamilika kujengwa ifaka Disemba 30 mwaka huu.


Waziri Jafo Ametoa agizo hilo leo alipotembelea  kukagua Maendeleo ya ujenzi wa nyumbahizo eneo la geza ulole ambapo amesema ameridhishwa na kiwango  Cha nyumba na malighafi iliyotumika katika ujenzi.

Amesema  nyumba hizo zinatakiwa zikamilie kwa muda huo ili watumishi wahamie  na kutimiza  agizo la Rais DKT Magufuli ambaye aliagiza ujenzihuo na kuchangia shilingi bilion mbili.

Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale akitoa taarifa fupi kuhusu mradi huo amesema  mradi wa nyumba za watumishi ulikuwa unahusisha ujenzi wa nyumba 20 lakini baada kushauriana na mtaalamu wa ujenzi  wakaongeza na kufikia nyumba 24 huku nyumba 2 zikiwa ni za ghorofa  na zakawaida zikiwa nyumba 22.

"Ujenzi  katrika nyumba  22 umefikia asilimia 61% nyumba zote zimekamilika boma Plasta kuzekwa bati mfumo wa umeme na maji, grilili za madirisha tayari zinachomelewa ,na ujenzi wa nyumba mbili za ghorofa ziko katika hatua ya Kenchi"Amesema Kiwale

Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11 Februari, 2020 alizindua Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam ambapo alizindua jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya  na jengo jipya la ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.

Wilaya ya Kigamboni inaeneo la kilometa za mraba 577.9 (hekta 57,786. ilianzishwa kwa tangazo la Serikali namba 462 la mwaka 2015 ikimegwa kutoka Wilaya ya Temeke kwa lengo la kusogeza karibu huduma kwa wananchi.

No comments