Ads

PBZ INAKUA KWA KASI YAJIPANGA KUONGEZA MATAWI ,YAJIVUNIA HUDUMA BORA

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah , akisiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa masoko na uendelezaji wa masoko wa Bank ya Zanziba PBZ Said Ally Mwinyigogo  alipo tembelea banada la PBZ 
Meneja wa masoko na uendelezaji wa masoko wa Bank ya Zanziba PBZ Said Ally Mwinyigogo akizungumza na waandishi wa habari  maonesho ya bidhaa za viwanda yanayofanyika katika viwanja vya maonesho ya biashara ya kimataifa Mwalimu Julius Nyerere Kilwa road jijini Dar es salaam   katika maonesho ya bidhaa za viwanda yanayofanyika katika viwanja vya maonesho ya biashara ya kimataifa Mwalimu Julius Nyerere Kilwa road jijini Dar es salaam  

N John Luhende 
Bank ya watu wa Zanzibar PBZ  imeishauri mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania  TANTRADE  kutenga eneo la mabanda  ambalo mabeki yatajenga ili inapofika kipindikipindi cha maonesho waweze kuonesha huduma zote zinazotolewa na Bank .

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa masoko na uendelezaji wa masoko wa Bank ya Zanziba PBZ Said Ally Mwinyigogo  katika maonesho ya bidhaa za viwanda yanayofanyika katika viwanja vya maonesho ya biashara ya kimataifa Mwalimu Julius Nyerere Kilwa road jijini Dar es salaam ambapo amesema PBZ imeshiriki maonesha hayo ili kwani shuguli za biashara zinaendana na huduma za kibenki.

"Tumekuwa tukishiriki maonesho maranyingi  ili kujitangaza watu bara  wajuwe tupo na huduma zetu tunazozitoa , tunamepata wateja wengi, Bank  hii makao makuu yake  yako Zanzibar tuna matawi 16 bara na Zanzibar  tuna huduma za usafirishaji fedha nje ambazo ni zaharaka na kuaminika   ,tunatoa mikopo nafuu  kwa wafanyakazi wa serikali "Amesema Mwinyigogo

Pia amesema Bank  hiyo inampango wa kufungua matawi maeneo mbali mbali ikiwemo kigamboni ,Tandika ,Arusha na Mwanza, Bank ya watu wa Zanzibar inatoa huduma za Bank ya Kiislam na nyingine ya kawaida.

Pamoja na hayo Meneja huyo alishukuru banda lao kutembelewa na Makomo wa pili wa Serikali ya mapinduzi Zanziba ambapo alipongeza PBZ  kwa kuongeza kwa kushiriki maonsho hayo na kuwataka wafanya kazi kuongeza bidii .

No comments