Ads

ASKARI POLISI WAUNGANA KUADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

 

Jamii nchini imetakiwa kuunga mkono serikali katika mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kutozipa nafasi aina zote za ukatili huo ikiwemo ukatili wa zamani na mpya .

Aidha imetakiwa kutilia mkazo mbinu za kupambana na ukatili ikiwemo kushirikisha wazee wa kimila,madawati ya kijinsia pamoja na viongozi wa dini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri  ya Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jumanne Shauri katika Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili huo yaliyofanyika yaliyofanywa na Mtandao wa Polisi Viwanja vya ndege na Kikosi Cha Anga -Airwing.

Alisema selikali pekee haiwezi kufanikiwa na kwamba jamii na wadau na mamlaka  husika zinatakiwa kuunga mkono serikali.

"Jamii inatakiwa kushiriki kupinga  vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo zinatakiwa kuunga mkono katika kushughulikia tatizo hilo ," alisema Elizabeth.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Kamishina Msaidizi wa Polisi Johari Said aliwahimiza washiriki wote wa maadhimisho hayo kuwa mabalozi wa kuhakikusha elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Mkuu wa Polisi Viwanja vya Ndege Ludegande Marabdu (SP) aliwashukuru wadau wote waliofanikisha tukio hilo.

Naye Kamanda wa Polisi Kikosi cha Anga Airwing Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marko Kusekwa alisema ukatili wa kijinsia kwa mwaka huu umepungua.

Maadhimisho ya siku 16 za kupunguza ukatili wa kijinsia yalianza November 25 na yatafikia tamati Disemba 10 mwaka huu.

No comments