SERIKALI YAONGEZA SIKU MBILI ZA MAONESHO YA NANENANE MWAKA 2020
Serikali imeongeza muda wa kumalizika kwa maonesho ya Kilimo Nanenane mwaka huu kwa siku mbili ili kutoa nafasi zaidi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kufika kwenye viwanja vya maonesho kote nchini.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa leo na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga (tarehe 04.08.2020) katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu alipoongea na waandishi wa habari.
“Muda wa maonesho ya Nanenane ni siku nane.Hata hivyo, mwaka huu sherehe zimechelewa kuanza baadhi ya kanda. Kulingana na mahitaji ya sherehe hizi kitaifa kilele kitakuwa siku ya tarehe 08 Agosti, 2020. Hivyo,tumeamua kuongeza siku mbili ya Jumapili na Jumatatu ili wananchi ambao hawakupata nafasi wapate kushiriki “ alisema Waziri Hasunga
Waziri Hasunga aliongeza kusema lengo la maonesho haya ni kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na wananchi wengi zaidi wajifunze kanuni bora za uzalishai mazao, matumizi sahihi ya pembejeo na viuatilifu,teknolojia mpya za uzalishaji mazao ili wazalishe kibiashara zaidi na kuwa na uhakika wa kipato.
“Kilimo ndio muhimili wa uchumi kwa watanzania walio wengi na inatoa ajira zaidi ya asilimia 58 na kuchangia malighafi za viwanda kwa asilimia 65 na pia kuchangia mapato ya fdha za kigeni kwa karibu asimilia 30” alisema Waziri Hasunga.
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga alitembelea banda la TABWA ( Tanzania Business Women Association ) na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kutoa elimu ya bima ya afya kwa wakulima na wafugaji husussan akina mama.
Aliwasihi vijana na akina mama nchini kote kuendelea kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ikiwemo kilimo na ufugaji ili wanufaike na huduma zitolewazo na taasisi za kifedha ikiwemo TABWA na mabenki.
Waziri huyo alitembelea pia banda la Wizara ya Afya upande wa Maendeleo ya Jamii ambapo amewapongeza kwa kuelimisha wakulima namna sahihi ya kupata chakula bora.
Alisema tatizo la lishe linasababisha wakulima na wafugaji nchini kutokuwa na afya bora licha ya uzalishaji mkubwa na utoshelevu wa chakula uliopo nchini bado watu wengi hawali chakula bora
“ Pongezi kwa Wizara ya Afya kwa kufundisha wakulima na wafugaji masuala ya lishe bora hapa Simiyu.Tatizo bado ni kubwa kwani watu wetu uwezo wao wa kula vizuri siyo mzuri” alisisitiza Waziri Hasunga
Waziri Hasunga ameagiza wataalam wa lishe nchini kote kutumia maonesho haya ya Nanenane kutoa elimu ya lishe bora ili Taifa liwe na watu wenye afya bora kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jamii Grace Mwanga alisema tatizo la udumavu kwa watoto nchini ni kubwa kutokana na kula vyakula visivyozigatia lishe bora.
“Tupo hapa Nyakabindi kutoa elimu ya lishe bora kwa wananchi ili kusaidia kaya kuboresha ulaji vyakula vyenye virutibisho vinavyotakiwa kuwezesha mwili kupata afya bora na watoto kutokuwa na udumavu” alisema Bi.Mwanga.
Kauli Mbiu ya Nanenane inasema “Kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi chagua viongozi
Post a Comment