Naibu Waziri Maliasili na Utalii Atoa neno Wahitimu Chuo Taifa Utalii, Awapongeza wadau kufanikisha Maendeleo.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Mahafali 17 ya Chuo hicho.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Mahafali ya 17 Chuo Cha Taifa cha Utalii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Taifa cha Utalii akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya mahafali ya 17 Chuo Cha Taifa cha Utalii.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Utalii wakiwa katika maandamano leo jijini Dar es Salaam ya kuingia ukumbini kwa ajili hafla ya mahafali ya 17 ya Chuo cha Taifa cha Utalii.
Afisa Mtendaji Mkuu Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi (wa pili kutoka kulia) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu wakiwa katika maandamano ya kuingia ukumbini kwa ajili ya hafla ya mahafali ya 17 ya chuo cha Taifa cha Utalii.
Baadhi ya Wahitimu wakiwa katika maandamano.
Baadhi ya Wahitimu Chuo cha Taifa cha Utalii.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Zaidi ya Wahitimu 100 katika Chuo Cha Taifa Utalii wametakiwa kuyafanyika kazi kwa vitendo waliojifunza katika kipindi chote cha masomo yao pamoja na kijiendeleza kimasomo katika ngazi mbalimbali za elimu ya juu ili waweze kuendana na soko la ajira la kimataifa katika Utalii.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Mahafali 17 ya Chuo cha Taifa Utalii, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu, amesema kuwa ni vizuri wahitimu wakajiendeleza kutokana na fani ya utalii inakuwa kila siku.
Mhe. Kanyasu ambaye ni mgeni rasmi katika mafali 17 chuo cha Taifa Utalii, amesema kuwa mafunzo waliyopata wanatakiwa kwenda kuyafanyia kazi ili yaweze kuleta tija katika maendelea ya Taifa.
"Nawapongeza wahitimu wote pamoja na kuwatakia maisha mema katika utekelezaji wa majukumu yenu" amesema Mhe. Kanyasu.
Mhe. Kanyasu amewashukuri wadau mbalimbali kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya Chuo cha Taifa Utalii.
Amesema kuwa uongozi wa chuo umefanya kazi kubwa katika kuendelea kujenga mahusiano mazuri na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Mhe. Kanyasu amesema kuwa ataendelea kutoa ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali katika chuo hicho.
Hata hivyo amefafanua kuwa sekta ya utalii hapa nchini imepewa kipaombele katika kuhakikisha inaendelea kuchangia kukuza uchumi.
"Sekta ya utalii inaongoza katika nafasi ya kutoa ajira pamoja kuongeza mapato katika fedha za kigeni na ndani" amesema Mhe.Kanyasu.
Ameeleza kuwa utalii hapa nchini unaingiza asilimia 25 za fedha za kigeni jambo ambalo linaonesha kuwa na tija katika taifa.
Mhe. Kanyasu amesema sekta utalii imeajili watu milioni moja hapa nchini na katika miaka ijayo itakuwa ni sekta inayotegemewa katika kuliingia taifa mapato.
Mwenyekiti wa Bodi Chuo cha Taifa cha Utalii Bw. Imani Kajula, amesema kuwa mfanikio ya chuo yametokana na mchango mkubwa kutoka kwa wazazi pamoja na wadau mbalimbali.
Bw. Kajula amesema kuwa anaamini wahitimu wanakwenda kuwa chachu ya maendeleo kupitia taaluma zao katika ukarimu na Utalii.
Amemuomba mgeni rasmi Mhe. Kanyasu kutatua changamoto mbalimbali kupitia mamlaka yake jambo ambalo litakuwa na tija.
"Bodi inaendelea mipango ya kuendelea kutafuta vyanzo vya mapato ili kutimiza malengo katika kuboresha utendaji" amesema Bw. Kajula.
Awali Afisa Mtendaji Mkuu Chuo Cha Taifa Utalii Dkt. Shogo Mlozi, amesema kuwa chuo kinaendelea na mipango katika kuhakikisha wahitimu wanaendelea kufanya vizuri katika soko la ajira.
Amesema kuwa licha ya jitiada mbalimbali chuo kinakabiliwa na changamoto ukosefu wa magari ya kufanyia kazi kwa vitendo katika kozi ya utalii ambayo inaitaji magari ya kutosha.
"Kuna ukosefu wa hoteli ya kufanyia vitendo kwa wanafunzi katika tawi la Arusha na mafunzo ya utalii hayawezi kutolewa kama miundombinu ya kujifunzia sio rafiki" amesema Dkt. Mlozi.
Dkt. Mlozi amefafanua kuwa kuna uhaba wa fedha za kutosha kwa ajili kuwajengea uwezo watumishi na wanafunzi katika kozi ya utalii na ukarimu ili waweze kupata uzoefu wa kimataifa.
"Chuo kinaendelea kutafuta fedha za kutosha kutoka kwa wahisani ili kuhakikisha tunapiga hatua katika mipango mbalimbali ya kimaendeleo" amesema Dkt. Mlozi.
Katika hatua nyengine Dkt. Mlozi ameeleza kuwa ili kuendelea kufanya vizuri katika kozi mbalimbali chuo kinaendelea kupitia mitahara katika kufanikisha wanatoa elimu bora.
Kwa upande wa Wahitimu wameonekana kuwa na furaha baada ya kumaliza masomo huku wakiwa na shauku ya kwenda kuitumia vyema elimu yao katika kuleta maendeleo kwa Taifa.
Wahitimu 144 katika fani mbalimbali Chuo cha Taifa Utalii katika fani ya ukarimu, mapishi, mapokezi, huduma ya chakula na vinywaji, utunzaji wa nyumba na ufuaji wa nguo pamoja na fani uokaji wamehitimu leo na kutunukiwa.
Lengo la Chuo cha Taifa Utalii ni kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia uweledi katika kutoa mafunzo ili kuwasaidia wanafunzi wake kufikia viwango vya juu katika fani ya ukarimu na utalii.

Post a Comment