Ads

Kyando: Amezitaka Halmashauri zote za Dar Es Salaam na Pwani kutoa huduma kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 2 usiku

Na Francisco Peter, Dar s Salaam

WANANCHI wa Mkoa wa Dar es Salaama pamoja na Mkoa wa Pwani  wanaodaiwa Kodi ya pango la Ardhi wametakiwa kulipa Kodi hizo kwa urahisi kwani wanaweza kulipa hata wakiwa nyumbani kwa Kupiga  *152*00# ambapo watapata maelekezo yote ya jinsi ya kulipa ikiwemo  kupewa 'control number' ambazo watalipa kwa njia ya simu au kwa njia  ya Benki.

Kwa mujibu wa Sheria ya ardhi kila mmiliki wa ardhi anapaswa  kulipa Kodi ya pango la ardhi kwa mkupuo au kwa awamu kila mwaka hivyo ni muda muafaka kwa wanaomiliki ardhi Mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani kulipa Kodi zao kabla ya tarehe ya mwisho ya kulipa Kodi hiyo ili kuepuka hatua  ambazo wanaweza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani na ardhi zao  kumilikishwa watu wengine au kuuzwa kwa nyumba zao ili serikali ipate  hela ya kufidia gharama ambazo mmiliki hakulipa kama Kodi ya Pango la ardhi kwa kipindi chote anachodaiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar Es Salaam Kamishna msaidizi,Kyando amesema kwa Sasa Ofisi za ardhi za halmashauri  zote  wanatoa huduma hadi saa mbili za usiku , siku zote za kazinakuwahudumia wananchi kwa urahisi.

Kyando amezitaka Halmashauri hizo zote za Dar Es Salaam na Pwani kutoa huduma kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 2 usiku kama Wizara  ilivyotoa agizo ili wananchi wengi wapate muda wa kulipa Kodi ya ardhi.

"Wamiliki watakaokaidi kulipa pango la Ardhi watafikishwa mbele ya mahakama na kwa mujibu wa fungu la 45 la Sheria ya Ardhi,taratibu za kisheria za  ubatilisho wa Miliki zao zitaendelea"amesema Kyando.

Siku moja Mara baada ya Wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoa siku 30 kwa wadaiwa wote wa Kodi ya pango la Ardhi kulipa Kodi hiyo, hii Leo  kamishna wa ardhi msaidizi Mkoa wa Dar Es Salaam na  Pwani Shukra  amesema kama wadaiwa wa Kodi ya Pango la Ardhi watashindwa kutumia simu  zao au kutembelea tovuti ya Wizara, wanaweza Kufika katika Ofisi za Wizara ya  Ardhi zilizopo mtaa wa Magogoni Jijini Dar Es Salaam au Kufika Katika Ofisi za Ardhi  katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani.

Aidha amewataka wananchi watumie njia walizoelekezwa na Wizara  ikiwemo kujikadiria wao kiwango Cha Kodi wanayotakiwa kulipa na kuzilipa  kabla ya tarehe husika ya mwisho ya kulipa Kodi hiyo ambapo Jana May 10,Wizara ilitoa siku 30 pekee.

Kwa upande wake Afisa Ardhi mwandamizi kitengo Cha Kodi Dar Es Salaam na Pwani, Seif Mahiza amesema wadaiwa wa Kodi ya Pango la Ardhi pia wanaweza kulipa Kodi  zao kwa kutembelea tovuti (website) ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi ambapo watapata taratibu zote za jinsi ya kulipa Kodi zao.


No comments