GIRLS APP YAWAKUTANISHA WASICHANA KUWASAIDIA KIUCHUMI
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Girls App kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani wametoa wito kwa watoto wa jinsia ya kike kukataa dhana zilizopo katika jamii ikiwemo kuonekana tegemezi na dhaifu.
Kuna dhana potofu iliyojengeka katika jamii nyingi za kiafrika kuwa mtoto wa kike hawawezi chochote na kwamba kazi yao ni kuolewa , kulea Watoto, pamoja na kufanya kazi za nyumbani.
Badala yake watumie teknolojia iliyopo ili kuondoa dhana hizo kwa kutimiza ndoto zao kwa kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Wilhelm Gasper, amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikiwakusanya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za serikali nchi kwa miezi sita lengo likiwa lengo likiwa kutafuta mawazo mbalimbali ambayo yatakwenda kutatua changamoto zinaikabili jamii.
Amesema kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa namna ya kutumia kompyuta kutengeneza tofuti ya mtandao baada ya hapo mabinti hao wanabuni miradi mbalimbali itakayoleta tija kwa jamii.
"Na Mara nyingi tumekuwa tukiandaa mikutano inayokutanisha wadau mbali mbali kwa ajili ya kutafuta mshindi aliyebuni miradi mizuri na kupewa zawadi ili wasichana wengine waige mfano huo hatimaye na wao wasibweteke bila ya kuwa wabunifu," amesema Gasper.
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Partterson aliwaasa wasichana kutumia teknolojia iliyopo ili kukuza uchumi wao na kuamini kwamba wao wanaweza na kwani wao ni nguzo kwa familia .
Pia mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne shule ya Kibasila Zahara Juma alisema wamenufaika vya kutosha kupitia kufundishwa kutumia kompyuta kwani wameweza kutengeneza tovuti mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.
"Hii kwetu ni fursa ya kipekee kabisa kukuza uelewa wetu na kuweza kujitegemea kiuchumi na tumekuwa tukikutana na wadau mbali mbali kupeana uzoefu ili kutatua changamoto zinawakabili," amesema Zahara.
Post a Comment