Ads

COSTECH NA DIT ZAINGIA MKATABA KUTAFITI NA KUTUNZA DATA ZA WANYA ,MAZINGIRA

 


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu na Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat Mohamed  wakibadilishana mikataa jijini dar es Salaam leo.

Mwamba wa habari
TUME ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ikishirikiana na Taasisi ya Teknolojia Tanzania (DIT) wamesaini mkataba na kujadili namna bora ya kuhifadhi, kuchapisha na kutumia data zinazuhusiana na baianuai(biodiversity) za mazingira na wanyama hapa nchini.

Akizungumza na wadau waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt.Amos Nungu amesema, lengo ni kutafiti, na kutoa elimu pamoja na kuendeleza sekta baianuai(biodiversity) inahusisha mgawanyiko wa maisha ya wanyama na mazingira.

Amesema lazima jitihada za makusudi zichukuliwe ili data ziweze kuhifadhiwa na tafiti ziweze kufanywa ambazo zitaelimisha sisi tuliopo na vizazi vijavyo.

"Kwahiyo tunamradi wa pamoja kati ya DIT na COSTECH, lakini sisi ni watekelezaji tuu, wadau wa mradi huo ni taasisi mbalimbali kulingana na majukumu yetu, tunaongelea mazingira na utalii nchini, sasa  kusudi jitihada zichukuliwe ili kuhifadhi, kutunza, na kufanya tafiti ambazo zinaelimisha, sisi tuliopo na vizazi vijavyo".

Dkt.Nungu amesema kuwa watafiti washirikiane pamoja katika kuibua data na taarifa kwaajili ya kuendeleza na kuhifadhi kwa maendeleo ya nchi.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat Mohamed amesema, mradi huu ni mhimu kwa taifa letu, ambao utatengeneza mfumo wa  kieletroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za baianuai(biodiversity), kwa kuwezesha kuapata taarifa za viumbe hai mbalimbali.

"Mradi wa kutengeneza mfumo wa kuhifadhi na kusambaza taarifa za baianuai(biodiversity) hapa nchini na kuwezesha  upatikanaji wa taarifa  hizi kwa wadau na kwa matumizi mbalimbali ".

Amesema taarifa za baianuai(biodiversity) ni mhimu kwa mipango ya kiuchumi na uhifadhi wa mazingira yetu.

"Taarifa za baianuai(biodiversity) ni mhimu kwa maendeleo ya taifa lolote,  maana bila viumbe hai hakuna maisha, bila mimea, wanyama na wadudu maisha ya binadamu yatakuwa hatalini maana ndio vyanzo vya  chakula, hali ya hewa nzuri, mvua na mahitaji mengine ya binadamu kama dawa".

Amesema kuwa tume ya Sayansi na Teknolojia kupitia wataalamu wake  iliandaa andiko la mradi likiwa na lengo la kufanya utafiti na kutengeneza mfumo wa kieletroniki wa kuhifadhi na kutoa taarifa za baianuai(biodiversity) ya Tanzania kwa wadau mbalimbali.

Hata hivyo Mwenyekiti wa taarifa za, baianuai(biodiversity) Tanzania, Profesa Pantaleo Munishi amesema baianuai(biodiversity)ni msingi wa maisha hapa duniani kwani kila kiumbe hai kinachoonekana ni baianuai(biodiversity).

"Baianuai(biodiversity) ni chanzo cha mahitaji mengi sana ya binadamu, mazao ya kilimo, mazao ya misitu, mazo ya majini, na vyakula aina mbalimbali pia ni chanzo cha uchumi"Alisema


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat Mohamed akizungumza wakati wa kusaini makubaliano kati ya DIT na tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu.


Baadhi ya viongozi wa DIT na COSTECH  waliofika kushuhudia utiaji saini katika mikataba hiyo. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu na Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat Mohamed wakisaini mkataa  leo jijini Dar es Salaam, kwaajili ya kutengeneza mfumo wa kielektroniki amao utahifadhi data za bainowai.





Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa kusaini makubaliano ya kutunza data na taarifa mbalimali za mazingira na wanyama.

No comments