MSAMAHA WA RAIS DKT JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI UWE ALAMA CHANYA YA MABADILIKO KATIKA JAMII
Na,Mwanaidi Awadh Kipingu.
Mnamo siku ya maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa taifa letu yani tarehe 9 mwezi wa kumi na mbili pale jijini Mwanza Mh Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli alitangaza hadharani kutoa msamaha kwa wafungwa wapatao 5533 ambao ni idadi kubwa ya msahamaha kutolewa kwa wafungwa katika historia ya taifa letu .
Kwa hakika msamaha huo wa Dkt John pombe Magufuli kwa wafungwa kuna funzo kubwa sana kwa jamii hasa tukiwa tunaelekea kumalizia mwaka huu wa 2019 na Rais ameonyesha mfano kuwa kuna haja ya watanzania wengine pia kuwasamehe wale watu waliowakwaza na hata wao kuomba msamaha kwa wale waliwakosea sababu kuna nguvu kubwa sana katika neno msamaha .
Nyuso za furaha kwa wafungwa hao ambao waliobahatika kupata msamaha wa Mh Rais Dk .Magufuli zilionekana katika magereza mengi nchini hasa kule Butimba jijini Mwanza wafungwa wapatao 79 waliweza kuachiwa huru katika gereza hilo
Tunafahamu fika kuwa idadi ya watu 5533 wanakuja uraiani kuungana na sisi hivyo kama wanajamii kuna tija kubwa ya kuwapokea watanzania wenzetu hao kwa roho nyeupe kabisa bila kuwa na kinyongo chochote kile na tuungane katika ujenzi wa taifa letu la Tanzania .
Lakini pia ujio wao uwe alama chanya katika jamii zetu kwani watumike kama mfano bora wa kuwaelimisha wanajamii hasa vijana wetu wadogo ambao wapo huko kwenye jamii umuhimu wa kutii sheria za nchi lakini kuishi kwa upendo.
Lakini pia kwenu nyinyi ndugu zetu mtokao gerezani ni matumaini makubwa kama jamii mtakwenda kuwa chachu na wazalendo kweli kweli kwa taifa letu lakini pia kwenye kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Dkt John Joseph Pombe Magufuli , yapo mengi yamefanyika uraiani mtakutana mafanikio makubwa nchini mfano Reli za kisasa za standard gauge, usafiri wa anga, barabara na maboresho makubwa ya huduma za afya nchini yote hayo ni mafanikio ya serikali ya awamu ya tano Viva magufuli viva nanukuu sifurahi kuongoza Taifa lenye watu wengi gerezani
Wanajamii kamwe tusiwatenge na wala kuwanyooshea vidole kwa ubaya bali tuwapokee na tushirikiane nao katika ujenzi wa taifa letu la Tanzania .
Nina imani yangu kabisa kuwa msamaha huo wa Dk John Pombe Magufuli utakwenda kuwa na alama chanya katika ujenzi wa taifa la Tanzania .
Mungu ibariki Africa ,Mungu ibariki Tanzania .
Viva vijana vivaaaaaaaa
Post a Comment