MEYA WA ILALA AZINDUA HARAMBEE KITUO CHA FAHARI
Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza katika mahafari ya kituo cha Fahari Day Care Wilayani Ilala Leo (Kulia)Mkurugenzi wa Kituo hicho Neema Mchau .
Mkurugenzi wa Kituo cha Fahari Day Care Neema Mchau akiongea katika mahafari ya ya kituo hicho(PICHA NA HERI SHAABAN)
Na Hery Shaban
Mwamba wa habari
MEYA wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amezindua harambee kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi mradi wa Kituo cha Fahari Day Care .
Harambee hiyo iliendeshwa na Meya Kumbilamoto ambaye alikuwa mgeni rsmi katika mahafari ya kituo hicho kilichopo Wilayani Ilala.
Katika harambee hiyo aliwaeleza WAZAZI siri ya mafanikio ya kushika nafasi ya tatu miaka mitatu Mfurulizo matokeo ya darasa la saba Halmashauri ya Ilala ambapo alisema baadhi ya shule wanafunzi wanakula kila siku chakula.
"Katika manispaa ya Ilala tunajivunia kiwango cha ufaulu kupanda kila mwaka kutokana na kujenga mazingira bora ya shule na kuweka utaratibu wa kuwapa chai wanafunzi na mlo wa mchana kila siku " alisema Kumbilamoto.
Aidha alisema halmashauri ya Ilala ikiwemo Kata ya Vingunguti wanafunzi wamewekewa utaratibu wa kupata mlo kila siku
Wanafunzi ambapo mwaka 2019 zaidi ya wanafunzi 23,000 wamechaguliwa darasa la saba .
Akielezea kituo hicho cha Fahari Day Care Kumbilamoto aliwapongeza kwa kuendeleza sekta ya Elimu katika Kata ya Gongolamboto wasitoze ada kubwa ili waunge mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli Mpango wa elimu bure .
Pia alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ilala itawasaidia Fahari Tuamke Maendeleo mchakato wa kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga shule ya Msingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau ,alisema kituo cha fahari kilianzishwa mwaka 2014 na kusajiliwa kwake 2016 dhumuni la kuanzishwa kwa kituo hicho kutoa elimu bora yenye malezi mema kwa watoto kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.
" Matarajio yetu mwaka 2020 tuanzishe darasa la kwanza tuwe na shule kamili inayomilikiwa na Fahari kwa sasa tupo katika mchakato wa kutafuta eneo La kujenga tupate eneo kubwa ndani ya wilaya ya Ilala " alisema Mchau.
Neema alisema katika Kata ya Gongolamboto wanashirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutoa misaada kusaidia shule za Serikali na kuandaa makongamano mbalimbali ikiwemo kuwaweka vijana Pamoja na kuwawezesha kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda.

Great job
ReplyDelete