Daktari aliye gundua Incubator ya kukuzia Watoto njiti aiomba Serikali kuongeza nguvu katika kuendeleza wabunifu.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Serikali imeshauriwa kuwekeza zaidi katika kuendeleza bunifu za wabunifu wazawa ili kuongeza teknolojia nchini na kuisaidia nchi kupunguza gharama kubwa zinazo tumika kununua mashine kutoka ughaibuni.
Ushauri huo umetolewa na Mbunifu wa Incubator ya kukuzia watoto njiti Dr Emmanuel Mushi, katika maonesho ya biashara ya bidhaa za zandani ambapo amesema kutengeneza Incubator hiyo inatumia gharama ndogo kiasi cha shilingi 500,000 ukilinganisha na zinazo uzwa kutoka nchi za ng'ambo ambazo zinagharimu milioni 25.
"Hapanchini kunaupungufu wa kifaa hiki na kuna hospitali zingine za Wilaya lakini hazina ,mimi nilikaa na kufikiria sana niliona kunashida tunapoteza watoto wanaozaliwa njiti na wale wanao zaliwa wamechoka kwa kupoteza joto, mwaka 2012- 2015 ilikuwa 25% na mwaka 2018 ilipungua na kufikia 21% ,nilitengeneza yakwanza na sasa nimetengeneza ya pili , wazungu walituficha vitu vingi na tulivinunua kwa bei kubwa hii ya kwangu inaviwango vya Dunia kulingana na viwango vya shirika la Afya Duniani"Alisema
Alisema Incubator ( Embrance warm ) hii yeye ni mtu wa pili duniani kubuni , Angle mark ni wa 409 kifaa hiki saidia wale wanao zaliwa wame ziba ulimi badala ya kuwadumbukiza kidole hii unamuwekatu na njia ya hewa inafunguka yenyewe pia amebuni Wallet warm ya kusafirishia Mtoto njiti inasaidia kuhifadhi joto la mtoto kutoka kijijini hadi Hospitali.
Kutokana na ubunifu huu Dkt Mushi ameishukuru Serikali kwa kutambua ubufu huo na anaendelea na kufuatilia uwezeshwaji wa serikali ili aweze kuanza kuzalisha vifaa hivyo hapa nchini na kusaidia watoanzania.
Akizungumzia jitihada za Serikali kuifanya nchi kuwa ya viwanda amesema mapinduzi ya kiviwanda kwa nchi yanapimwa kwa kuwa na teknojia iliyo nayo nchi na namna inavyo saidia wabunifu bila kujali ni vya aina gani na kutoa wito kwa Serikali kuwekeza zaidi katika bunifu.
"Mao setum wakati wake alisaidia wananchi wake kuwekeza katika teknolojia ndyiyo maa leo mnaona wachina wanatuuzia kila kitu hadi vijiko , kwasa wachina na wazungu baada ya kuoa hii wamekuwa wakihangaika wameniita Amerika ,Ujerumani na kunawachina wamesema wanaweza kuingia makubaliano wajenge kiwanda hapa nchini"Alisema .
Kwa upande wake kaimu afisa habari wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Deusidedith Leonard amesema ,Tume hiyo imekuwa ikiwasaidia wabunifu kuhifadhi na kuendeleza bunifu zao na pia wamekuwa wakiendesha mashindano yakitaifa ya wabunifu (MAKISATU) ili kuibua vipaji.
"Mtakumbuka jumalililopita tuliendesha warsha kubwa ya wabunifu 60 walishinda mashindano ya mwaka jana na tume waahidi kuendeleza bunifu zao ambapo tumewapa elimu na kuwashika mkono kwa kuwapa fedha za kuendeleza bunifu hizo na si fedha tu bali tuna walea na kuwanunulia vifaa.
Amewataka watafiti na wabunifu kuendelea kujitokeza ili wapewe elimu zaidi ya kulinda kazi zao ili teknolojia zao zisiweze kuibiwa na wajanja kuwahi kusajili na wao kupoteza haki zao.
Post a Comment