Ads

WAZIRI DK MPANGO ANATARAJIWA KUTUNUKU VYETI NA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA CMSA.




Na John Luhende
 Mwamba wa habari
Waziri wa fedha na mipango  Dkt Philp Mpango, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutunuku veti kwa washindi wa shindano la wanafunzi na taasisi za vyuo vikuu na elimu ya juu  ,ambalo limevunja rekodi  na kuvuka lengo ambapo washiriki waliotarajiwa ni 7,000  lakini wakafika 16,625.

Hayo yamebainishwa na afisa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya mitaji ya dhama Tanzania (CMSA), Bw Nicodemas Mkama  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam , ambapo alisema  taasisi hiyo ina wajibu wa kusimamia na kuendeleza masoko .

''Taasisi hii inayo ina majukumu makubwa mawili  kusimamia na kuendeleza masoko ,katika kutekeleza hayo tuliandaa shindano hilo  linalohusishwa teknolojia ya simu kuwafikia wanafunzi na tumepata mafanikio makubwa sana "Alisema

Mukama alisema ,mshindi wa kwanza wa shindano hilo anatapata zawadi ya shilingi 1,800,000,mshindi wa pili 1,400,000  mshindi wa tatu atapata shilingi 800,000 mshindi wa nne atapata shilingi 400,000 na wengine  20 watakao pata alama za juu watapatiwa shilingi 250,000.
Alisema  ,washindi hao 1/3 ya feha hizo watatakiwa kuziwekeza katika hisa za kampuni zilizo orodheshwa katika soko la hisa la Dar es salaam.

Miongomi mwa watakao pewa tuzo ni pamoja na  watendaji katika masoko ya mitaji watakao kidhi vigezo vya kimataifa ambao wanaweza kutoa huduma hizo ulimwengu kote, hiyo ni kutokana na mafunzo yaliyotolewa  kwa kushirikiana na taasisi ya  Chartered Institute For Security Investment ya nchini uingereza.

No comments