Ads

Wachungaji wajitokeza kubariki uchaguzi serikali za mtaa

Mchungaji Daudi Mashimo (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Mungu kutoka Makanisa mbalimbali wamekutana kwa ajili kuombea uchaguzi wa serikali za mtaa ufanyike kwa amani ambao unatarajia kufanyika Novemba 24 mwaka huu.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Wamesema  kuwa  ni busara vyema vyote vya siasa vishiriki uchaguzi serikali za mtaa ili wananchi wapate fursa ya kupiga kura kwa kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Wamesema wagombea kutoka vyama vya upinzani waendelea kufanya kampeni za uchaguzi na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mtaa.

Akizungumza kwa niaba ya Wachungaji wenzake Mchungaji Daudi Mashimo, amesema lengo lao ni kuiombea nchi ili iwe na amani na wataendelea kusimama na kuiombea nchi.

Amesema kuwa ni vyema watu wote kuungana kwa pamoja kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa amani ili kupata viongozi bora.

No comments