Ads

Bondia Philippines Tinampay atua Dar na Timu Manny Pacquiao kumkabili Mwakinyo

Bondia Arnel Tinampay akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kmataifa wa Mwalimu Nyerere.

 Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam
Bondia Philippines Arnel Tinampay amewasili leo kwa ajili ya pambano la kistoria kati yake na bondia  Mtanzania Hassan Mwakinyo linalotarajia kufanyika Novemba 29 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.

Bondia huyo Tinampay amesema kuwa amekuja leo siku 11 kabla ya pambano hilo kwa ajili kuzoea mazingira ya jiji la Dar es Salaam kwa sababu kuna utaofauti mkubwa na nchini kwao.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Bondia Tinampay, amesema kuwa licha ya ubora wa Mwakinyo ametamba kumpinga mpinzani wake katika raundi za awali.

"Nimejiandaa vizuri kuelekea pambano hilo, naamini nitafanya vizuri kwa kumpiga mpinzani wangu" amesema Tinampay.

Amesema kuwa amekuja nchini Tanzania kuwakilisha timu ya Bondia Manny Pacquiao katika pambano hilo, huku akibainisha lazima afanya vizuri.
Promota Jay Msangi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Promota wa pambano hilo, Jay Msangi amesema Tinampay atafanya mazoezi ya wazi Mlimani City na Mbagara jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Tanga ilipo kambi ya Mwakinyo ambako pia atafanya mazoezi ya wazi kisha kurejea Dar es Salaam tayari kwa pambano.

"Maandalizi ya pambano yamekamilika na yamekwenda vizuri ikiwa ni pamoja na Tinampay tayari amewasili katika jiji la Dar es Salaam" amsema Msangi.

Bondia Tinampay ameambatana na kocha wake, Victor Man 'On fire' atafanya mazoezi ya wazi jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Tanga, ambako atafanya kwenye uwanja wa Tangamano na kisha kurejea Dar es Salaam kumkabiri Mwakinyo.

Bondia huyo ametamba kumpiga kwa Knock Out, Mwakinyo katika ardhi ya Tanzania akisisitiza kuwa anafahamu ubora wa Mtanzania huyo ambao amesema ana punchi nzito.

Tinampay na Mwakinyo watazichapa Novemba 29 pambano la raundi 10 la uzani wa super welter litakalopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiombwa kuwa mgeni rasmi.

No comments