DC JOKATE AZINDUA MRADI WA MAJI MARUI KISARAWE
Na Heri Shabani
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo jana amezindua mradi wa maji safi na salama kwa wakazi wa Marui Mipera Wilayani Kisarawe.
Mradi huo wa Maji umfadhiliwa na Shirika la Reflection Foundation (ARF)kwa kushirikiana na Ghulam Hussein Electra Chertable .
Akizindua mradi huo Jokate alitoa onyo kwa watumiaji maji hayo wasitumie kama chanjo cha Biashara kwakujinufaisha wao mradi huo ni kwa ajili ya jamÃi nzima.
"Zaidi ya wakazi 4000 wa kijiji ichi Marui watanufaika na mradi huu wa maji serikali yetu sikivu imewapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji tunawashukuru wafadhiri wetu waliowezesha mradi huu "alisema Jokate
Jokate alisema mradi huo ni mkubwa mpaka ukikamilika utakuwa umegharimu shilingi milioni 69 chini ya ufadhili wa Reflection Foundation (ARF)kwa ushirikiano wa Ghulam Hussein Erectra Charitable.
Alisema alisema katika kijiji hicho kwa sasa kero imekwisha mradi huo ukikamilika kisima kina urefu wa mita 200 .
Katika uzinduzi wa mradi Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo alikabidhiwa na
Balozi wa shelisheli ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la Afrika Reflection Foundation (ARF) MERY VAN POOL pamoja na mkurugenzi Taasisi Ghulam Hussein NAFEESA JANMOHAMMED.
MWISHO
Post a Comment