Ads

WAJASILIAMALI KIGAMBONI WAJAZWA MAPESA .

Na John Luhende

Vikundi vipatavyo   88 vya wajasiliamali  katika  Halmashauri ya Manispa ya Kigamboni  vimepatiwa  mkopo wa fedha jumla ya shilimngi milion 300  huku milioni 200 ikiwa ni sehemu marejesho ya  mkopo kutoka vikundi vya akinamama ,vijana akina mama na walemavu.

Akizungumza katika hafla ya kutoa mikopo hiyo iliyofanyika Kibada, mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  Mhe. Sarah Msafiri amewataka wafanyabiashara na walipa kodi wilayani humo kulipa kodi kwa wakati  ili kuongeza mapato na kiwezasha halmashauri kuendelea kutoa mikopo .

Aidha amevipongeza  vikundi kwa kufanya marejesho kwa wakati  huku akitolea mfano kikundi cha gonga gonga kinacho jishughulisha na utengenezaji  samani zandani (Sofa )  kuwa kimekuwa cha kwanza kukamilisha marejesho na kuenelea kuwa na sifa ya kuendelea kupewa mkopo na kuvitaka vikundi vyote kuiga mfano huo.

Akizungumza na vikundi vya akinamama DC Msafiri amewataka akinamama kuwafundisha biashara mabinti na wategemezi wao kuliko kukaa bila kuwa na shughuli za kufanya  jambo ambalo amesema halileti picha nzuri kwa maisha yao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ng'wilabuzu Ludigija, amesema mwamko wa vijana wa kiume kuchukua mikopo umeongezeka  na mkopo huo unatolewa kwa haki bila upendeleo.
"Tumejipanga vizuri tunakamati yetu inayoshughulikia mikopo  hakuna mtu anaye pata mkopo kwa upendeleo tuna tenda haki ,ninacho waomba wanufaika wote wa mkopo mlichukua leo mkawe waaminifu katika marejesho ili na wenzenu wengine wakakopeshwe ''Alisema

Kata ya mjimwema  imeonekakana kuwa na vikundi vingi kuliko kata nyingine ,Diwani wa kata hiyo Selestine Maufi anaeleza siri ya mafanikio hayo kuwa hamasa aliyoifanya na viongozi wa kata hiyo .
"Katika vikundi 88 Mjimwema tuanavikundi 26 , napenda kuwapongeza sana wanachi kwa kuitikia nikweli tumewahamasisha sana naomba na wenzetu katika kata zingine mchangamkie mkpo huu serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwasadia wananchi wake  jitokezeni mikopo hii haina riba"Aalisema Maufi.

Moja kati ya vikundi vilivyo pata mkopo huo ni kikundi cha walemavu  Wasiyo ona ,Diana  Mapunda ambaye ni mmoja wa wanufaika kutoka kundi hilo ameishukuru serikali kwa kuwajali walemavu  huku amwaga pongezi hizo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaona nao kuwa ni sehemu ya wananchi wake wanastahili kupewa mkopo.

"Sisi vipofu tuna dharaulika sana hata ukimwambia mtu kwa nachukua mkopo anashangaa utarejeshaje, lakini  nataka niwaambie sisi tutarejesha vizuri tunashughuli zetu tunazofanya "Alisema Diana.

No comments