Simba yaongeza wawili wapya
Katika kuhakikisha wanafanikisha kukamilisha mfumo wa mabadiliko ndani ya klabu ya Simba, Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mohammed Dewji ‘Mo’ imetangaza wawili wapya ndani ya uongozi.
Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe amesema kuwa, klabu hiyo imepanga kuimalisha nafasi mbalimbali za uongozi ambapo awali ilitangaza nafasi 11 ikiwemo ya Mkurugenzi wa Wanachama na mashabiki ambayo tayari imechukuliwa na Hashimu Mbaga.
“Miongoni mwa nafasi hizo ni hii ya mkurugenzi wa wanachama na mashabiki ambayo ameipata ndugu Hashimu, aliomba pamoja na watu wengine lakini yeye amefanikiwa kukidhi vigezo.
“Kazi yake kubwa itakuwa ni kuhakiki wanachama wa Simba na kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa wanachama hivyo atakuwa karibu nao na mambo yote yatakayowahusu wanachama
atahusika nayo yeye.
“Kwa upande wa Rispa Hatibu yeye nafasi yake ni ya kuteuliwa kuwa msaidizi wa mtendaji mkuu wa bodi, lengo likiwa ni kuweza kufikia malengo ya mabadiliko,” alisema Kashembe.

Post a Comment