Ads

SERIKALI YAITAKA CMSA KUENDELEA KUBORESHA MPANGO WA KUTOA ELIMU YA MASOKO YA MTAJI VIJIJINI.


 
Na John Luhende 
Mwamba wa habari
Serikali  imeitaka  Mamlaka ya ya masoko ya mitaji na dhama Tanzania CMSA kukabiliana na  chanamoto mbalimbali kwa kuboresha mpango wake wa kutoa elimu kwa umma na huduma zaidi  kwa makundi mbali mbali katika kutekeleza jukumu kubwa la  mamlaka la kuendeleza  masoko ya mitaji nchini  hasa vijijini



.Hayo yamebainishwa na Naibu waziri Ofisi ya Rais  tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege   wakati wa  hafla ya kutunuku veti na zawadi kwa washindi wa shindano la wanafunzi na taasisi za vyuo vikuu na elimu ya iliyofanyika jijini Dar es slaam ambapo wanafunzi  16,275 .walishiki shindano hilo .
Alisema  Serikali kupitia Sekta masoko ni muhimu katika upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa makampuni na husaidia umilikishaji wa umma  kwa njia za uchumi  wa nchi kadiri  Taifa linavyosonga mbele  katika utekelezaji wa sera ya uchumi  wa Viwanda mahitaji ya fedha za kutekeleza  miradi ya maendeleo hususani miundo mbinu  unaongezeka .
Kaika kufanikisha azma hii kunahitajika wataalamu wa kutosha katika masoko ya mitaji wenye weledi wa hali ya juu ,uwepo wa wataalamu wazalendo na walio bobea  unasaidia katika kuhakikisha  maslahi ya Taifa yanalindwa.
"Nimatumaini yangu kuwa ninyi mlio tunukiwa vyeti siku yaleo  mtatoa mchngo mkubwa  katika kufanikisha  azma ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda "Alisema 
Pamoja na hayo Kandege alisema ,Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inatambua na kuthamini juhudi zinafanywa  katika kuongeza uelewa kuhuhusu masoko ya mitaji  na kuwawezesha wananchi   kujiletea maendeleo.
Awali mtendaji mkuu wa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhama Tanzania (CMSA), Bw Nicodemas Mukama   alisema  kupita shindano hilo  mamlaka imeweza kuwafikia wanafunzi 16,275 ,tofauti na matarajio yaliwekwa ya kuwafikia wanafunzi 7,000.
Wanafunzi 80 kutoka  kutoka vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu  walio pata alama za juu katika shindano  la maswali na majibu ni  wavulana 20 wasichana 20  vile vile katika shindano la Insha  wavulana 20 na wasicha 20 kati ya washiriki 16,275 sawa na asilimia 0.5 ya washiriki wote.
"Mshindi wa kwanza wa shindano hilo amepata zawadi ya shilingi 1,800,000,mshindi wa pili 1,400,000  mshindi wa tatu amepata shilingi 800,000 mshindi wa nne amepata shilingi 400,000 na wengine  20 walio pata alama za juu wamepatiwa shilingi 250,000 "Alisema Mkama.
Washindi 12  yaani wavulana 6 na wasicha 6 walio[pata alama za juu zaidi watagharimiwa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ili kujifunza maswala ya masoko ya mitaji ikiwa ni pamoja na masoko ya hisa  na kampuni kubwa zinazohusika na utoaji huduma katika masoko ya mitaji hapa nchini na nchini Namibia

No comments