Ads

MD SHAILA LUKUBA APANIA KUPANDISHA MANISPAA YA MOROGORO KUWA JIJI.





Na John Luhende
 Mwamba wa habari 
Uongozi wa Manispaa ya Morogoro wakiwemo Mkuu wa wilaya ,Mkurunzi ,Mstahiki Meya ,Madiwani na baadhi ya  wakuu wa idara mbalimbali  wamefanya ziara ya  mafunzo jijini Dr es salaam katika Manispaa ya Ilala kujifunza namna bora ya kukusanya kodi  ili kuongeza mapato ya Manispaa hiyo.

Akizungumza na Mwamba wa habari , Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Shaila Edward Lukuba  alisema  lengo la ziara hiyo ni kujifunza mbinu bora zaidi ili kuongeza mapato na kuifanya Morogoro kuwa Jiji.

Alisema ,katika Manispaa ya Morogo kumekuwa na udanganyifu  hasa kwa wamiliki wa hoteli kwa kudanya mapato halisi  , hapa anaeleza namna alicho baini baada ya kufanya ziara katika baadhi ya hoteli na nyumba za kulala wageni.

"Mfano nlienda katika hotel moja wageni wamelala 17 kwetu kimeletwa kitabu kinaonesha wameandikwa wame lala wageni  6 tu, baada ya kumbana mhudumu  akasema hao wengine walikuwa ndugu wa Meneja nikambana zaidi na kumwambia nitampleka Polisi akabadilika  akasema nikweli nilikuwa nakudangaya, "Alisema

Pamoja na hayo Lukuba amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro kulipa ili kuiwezesha serikali kutekeleza shuguli za maendeleo.

''Natoa wito kwa wanamorogoro tulipe kodi kwa manufaa ya maendeleo ya wanamorogoro  kuna ujenzi wa madarasa ,Elimu bure  ujenzi wa hospitali hata sisi tulisoma kwenye madarasa waliyo jenga mababu zetu  tusipojenga nani atakuja kujenga? "Alisema

Spia Komanya ni diwani wa kata ya Mafiga  na mwenyekiti wa kamati ya  kudumu ya  huduma za uchumi , elimu na Afya  amesema ,ziara hiyo ina manufaa makubwa kwani wamejifunza  namna wenzao walivyo fanikiwa  na kwamba mbinu hizo zitawasaidia kundeleza Manispaa yao.

No comments