Ads

TCRA yaongeza muda wa usajili kwa Wananchi wa Makambako hadi Desemba 6.

Kufuatia na kujitokeza kwa wingi kwa wakazi wa Makambako na viunga vyake vya jirani katika zoezi la kupata namba za vitambulisho vya taifa na kusajili simu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na watoa huduma wote wa makampuni ya simu wameongeza muda wa zoezi hilo  ambapo  sasa zoezi hilo utafanyika kwa wiki  nzima kuanzia Desemba  2 hadi 6 2019.

Akizungumzia  maendeleo ya zoezi hilo linaloratibiwa na TCRA mkuu wa kanda ya Nyanda za juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopata huduma za msingi kwa urahisi hivyo kuongeza huko kwa siku kunalenga kutekeleza  malengo hayo.

Amesema huo ni muendelezo wa kampeni ya "Mnada kwa Mnada, Karibu tukuhudumie" iliyoanzishwa na kuratibiwa na TCRA  na kushirikisha wadau wengine  inayolenga kutoa elimu ya utumiaji bora na salama wa huduma za mawasiliano  na kuhamasisha usajili wa laini kwa kutumia namba za vitambulisho vya taifa.

No comments