NHIF YALETA HAUWENI MATUMIZI BIMA YA AFYA, MHE. MAKINDA AZINDUA RASMI MATUMIZI YA VIFURUSHI
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mhe. Anne Makinda akikata utepe wakati wa uzinduzi wa vifurushi vipya vya bima ya afya leo jijini Dar es salaam Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Bernard Konga na kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Tryphone Rutazamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Mhe. Peter Serukamba.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Watazania wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuchagua kifurushi jambo ambalo ilitasaidia kuleta hauweni wakati mtu anapotaka kupata huduma ya matibabu ya afya.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuzindua vifurushi vya bima ya Afya, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mhe. Anne Makinda, amesema kuwa wakati umefika kwa kila mtanzania kuwa na bima ya afya kupitia vifurushi katika mfuko huo.
Mhe. Makinda amesema kuwa mfumo huu wa NHIF unampa fursa kwa kila mtanzania kuwa na kadi ya bima ya afya kwa gharama nafuu ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mhe. Anne Makinda akikabidhi kadi ya bima ya afya mara baada ya kuzindua vifurushi vipya vya bima ya afya vya najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
"Sisi kama bodi lengo letu kufanya kazi kwa karibu na watoa huduma ya Afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyobora" amesema Mhe. Makinda.
Ameeleza kuwa mpango wa vifurushi vya bima ya Afya utamwenzesha Kila mtanzania kujiunga kulingana na mahitaji yake kwani kwa mtu mmoja anatakiwa kulipa Sh 192,000 kwa mwaka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha za pamoja na makundi mbalimbali na wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi leo jijini Dar es Salaam.
Amefafanua kuwu alikuwa mtu mmoja alikuwa analazimika kutoa Shiliingi millioni moja na laki tano jambo lilikuwa ni changamoto.
Katika hatua nyengine amewataka watoa huduma kutumia kauli nzuri kwa wateja ambao wanatumia Bima ya Afya ili waweze kuvutuwa na huduma hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Temeke (DC) Felix Lyaniva, amesema kuwa vifurushi vya mfuko wa bima ya afya umekuja wakati mwafaka kutokana na changamoto zinazowakabili wananchi.
Dc Lyaniva amesema kuwa kutokana fursa ya bima ya afya, wamepanga ratiba ya kuanza kuhamasisha makundi mbalimbali ili waweze kujiunga na kulingana na mahitaji yao.
Post a Comment