Ads

MANISPAA YA ILALA WAZINDUA SHERIA YA OMBAOMBA NA HERI SHAABAN


HALMASHAURI ya Ilala imezindua sheria maalum ya  ombaomba ambayo inazuiya wananchi kutoa pesa kuwapa ombaomba barabarani.

Akizungumza  katika uzinduzi huo Afisa Ustawi wa Manispaa ya Ilala Joyce Maketa alisema kitendo cha Wananchi kutoa fedha kuwapa ombaomba ni kosa kisheria hairusiwi mtu yoyote kutoa pesa kuwapa  omba omba .

"Manispaa yangu ya Ilala kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Ilala , leo tumezindua sheria ndogo ndongo za kudhibiti ombaomba za halmashauri "alisema Maketa.

Maketa alisema sheria hizo zitatumika katika eneo lote  lililo chini ya Mamlaka ya halmashauri ya Ilala Afisa Mtendaji wa Kata au Mtumishi yeyote wa Umma aliyejiriwa anatakiwa kutekeleza majukumu yake  kwa kufuata sheria hizo..

    Alisema halmashauri inaweza kumteua Wakala ambaye atasimamia jukumu la kudhibiti ombaomba kwenye sehemu au eneo lote la halmashauri ya Ilala kwa niaba ya halmashauri.

Aidha alisema kila mkazi wa manispaa ya Ilala analo jukumu la kudhibiti ombaomba katika eneo analoishi kwa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi  ,Afisa Mtendaji wa Kata au Afisa Mtendaji wa Mtaa.

Alisema sheria hiyo mpya   mtu yeyote atakayekutwa mtaani au eneo la wazi na Afisa au Wakala akiomba fedha au chakula kwa mtu au watu wengine atahesabika naye ni ombaomba.

Pia ukikutwa au ukionekana ukiomba mtaani au kukaa ,kusimama au kulala mitaani ,eneo la wazi na kupiga mziki ili kuomba kwa kuonesha kidonda,ulemavu  utahesabika na wewe ni ombamba.

Kwa upande wake Mwanasheria  wa Ilala Isack Mudo alisema mda mrefu kulikuwa amna sheria ya kudhibiti ombaomba kwa sasa halmashauri imeunda sheria hiyo OMBAOMBA akikamatwa anafungwa .


Mwanasheria Isack alisema kwa sasa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ameanda mafunzo hayo kwa ajili ya kuwapa elimu wadau mbalimbali  Mafisa Watendaji ili wafahamu elimu hiyo waipeleke ngazi ya jamii.

No comments