Wadau wa Mazingira wasisitiza wanachi kufuata sheria za Mazingira
Mwamba wa habari
Halmashauri ya Mnispaa ya Ilala imesema imeongeza uwezo wauondoshaji taka mjini baada ya kununua magari ya kisasa ya kuchakata taka (compactor ) jambo ambalo litasaidia kuweka mazingira ya jiji kuwa safi.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa Idara ya uhifadhi mazingira na udhibiti takangumu Manispaa ya Ilala ,Abdon Mapunda wakati akizungumza katika warsha ya wadau wa mazingira na kuwataka wananchi wanaoingia manispaa ya ilala kuwa makini wasitupe taka hovyo kwani kuna askari wanao kamata watu wanao kaidi sheria .
''Suala la elimu ni mwendelezo na imetolewa na tunaendelea kutoa elimu kupitia vyombo mabalimbalivya habari ,na tumekuwa tukiwaaelimisha kuwa utupaji wa taka unachafua mazingira na unasababisha gharama katika Manispaa "Alisema
Alisema, Ilala imekuwa safi kutokana na makampuni yaliyo pewa zabuni pamoja na manispaa yenyewe kuongeza uwezo kwa kununua vitendea kazi .
Mapunda ,alisema wataendelea kusimamia sheria kwa kuwakamata na kuwatoza faini watu wote wanao tupa taka hovyo na kuwataka kuwasiliana na uongozi wa Manispaa ya Ilala wanapohisi hawajatendewa haki.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Climate Change Forum CC ,Rebeca Muna alisema usimamizi wa sheria za mazingira unatakiwa kutiliwa mkazo ili kuwabana wachafuzi wa mazingira .
"Wafanyabiashara wamekuwa wajanja wameutumia mwanya wa vifungashio kuendelea kutumia mifuko ya plastik , watu wanafahamu kuwa hawapaswi kutumia mifuko hii elimu iendelee kutolewa kwa wafanya biashara ili wafahamu madara "Alisema
Mabadiliko ya Tabia ya nchi yameikumba dunia na Tanzania na nchi zingine zinashindwa kuhili athali za kimazingira kwa sababu ya uchache wa lasili mali na kumekuwa na athali za mafuriko ,ukame na ongezke la magojwa yanayochochewa na joto na ukanda wapwani baadhi ya maeneo yamefunikwa na maji kuharibika kwa vyanzo vya maji kama maji yalikuwa matamu kwa kunywa sasa yamebadilika kwa kuwa na kiwango cha chumvi.
Abdala Mbena ni Meneja wa kampuni ya Greeni westpro ana shauri wanasiasa kuwa himiza wananchi kulipa ada za taka kwani wasipo lipia kazi inakuwa ngumu.
"Tunapata ugumu sana pale wananchi wasipo shiriki kulipa taka ,unapolipia ndiyo huduma hii tunaendelea kuzifanya tuna ona baadhi ya watu wanapa taka hovyo wanasabasha kuziba kwa mitaro ya maji na kuongezeka kwa mafuriko , wanasiasa watusaidie kuelimisha wananchi badala ya kuwakingia kifua na kujiona kuwa hawastahili kulipa "Alisema.
Post a Comment