Ads

Balozi wa Italia Tz azungumiza Wiki Ya Vyakula.

Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko kutoka Hoteli ya Serena Bw. Seraphin Lusala.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Ubalozi wa Italia nchini Tanzania unatarajia kushiriki wiki ya Vyakula vya Italia itakayoanza Novemba 25 hadi 30 mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Katika wiki ya vyakula vya Italia wadau mbalimbali watakaoshiriki watapata fursa ya kujua utamaduni wa Italia pamoja na vyakula mbalimbali ambavyo wanapenda kuvitumia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni, amesema kuwa wiki ya chakula cha Italia itafanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Balozi Mengoni, amesema kuwa anafuraha kubwa kuwaalika wadau mbalimbali kushiriki katika kula chakula cha Italia kuanzia novemba 25 hadi 30 mwaka huu ili kuona vyakula bora kutoka nchini Italia.

"Katika wiki ya chakula cha Italia katika hoteli ya Serena kutakuwa na wapishi wawili ambao watakuwa wanapika vyakula mbalimbali vya Italia" amesema Balozi Mengoni.

Balozi Mengoni amefafanua kuwa katika wiki hiyo wanafunzi wa Chuo Cha Taifa cha Utalii watapata fursa ya kufunishwa namna bora ya kuandaa chakula cha Italia.

Ameeleza kuwa siku ya novemba 30 kuanzia saa 5 asubuhi kutakuwa na chocolate kwa kila mtu, ambapo mtaalamu wa kutengeneza chocolate Bi Angela De Luca atafundisha jinsi kutengeneza kwa kutumia bidhaa za Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko kutoka Hoteli ya Serena Bw. Seraphin Lusala, amesema kuwa ni fursa kubwa kushiriki wiki ya Vyakula vya Italia katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutangaza Utalii.

Bw. Lusala amesema kuwa kupitia wiki hiyo watajifunza mambo mbalimbli ikiwemo utamaduni wa Italia ambayo inaweza kuongeza idadi ya watalii nchini.

"Tanzania kuna watalii kutoa nchini Italia, wengi wapo Zanzibar ambapo kuna hoteli ya Serena" amesema Bw. Lusala.


No comments