CUF Yatoa Maazimio Baraza la Uongozi Taifa, Prof. Lipumba azungumzia maandamano.
Chama Cha Wananchi (CUF) kimesema hawana mpango wa kufanya maandamano siku ya uchaguzi wa serikali za mtaa Novemba 24,2019 na badala yake kitaendelea na shughuli zake za kukijenga chama.
Kauli hiyo kutoka CUF inakuja baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa chama hicho kinampango wa kufanya maandamano kipindi cha uchaguzi wa serikali za mtaa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti Taifa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipokuwa akitoa taarifa ya maazimio ya Baraza la Uongozi la Taifa katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika Novemba 13 hadi 15.
Prof. Lipumba amesema kuwa chama hicho akina mpango wowote kufanya maandamano licha ya kujitoa katika Uchaguzi wa serikali za mtaa ambao unatarajia kufanyika novemba 24 mwaka huu.
"Hatuna mpango wa kufanya maandamano, kwani yana utaratibu wake wa kufatwa na si kinyume na utaratibu huo ...kwani ni lazima kuandika barau pamoja na kupata kibali kutoka sehemu husika"amesema Profesa Lipumba
Profesa Lipumba alifafanua kuwa chama hicho kwa sasa kimejikita katika kukijenga chama,kuimarisha matawi ili kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Amesema kuwa katika kipindi hiki ni vyema wanachama wa CUF kutokukata tamaa kwa yote yaliotokea katika uchaguzi wa serikali za mtaa na badala yake wasimame imara na kuungana na chama hicho kudai Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.
"Tunawapongeza wanachama wa CUF waliojitokeza kuweka nia kugombea nafasi za Uongozi katika serikali za mtaa, tunaomba msikate tamaa kwa yaliotokea bali tuungane kwa pamoja na kufanya ujenzi wa chama nchi nzima utakaohakikisha kuwa mpango uliotumiwa kuengua wagombea wetu haufanikiwi tena katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020"amesema Profesa Lipumba
Akizungumzia uchumi wa Tanzania Profesa Lipumba amebainisha kuwa CUF linafahamu kuwa ongezeko la ujazi wa fedha umepungua katika kipindi cha awamu ya tano.
Amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Benki kuu Tanzania zimeonesha kasi ya ongezeko la ujazi umepungua kutoka asilimia 15.6 kwa mwaka 2015 na kufikia 0.3 kwa mwaka 2016, 2017 ilikuwa ni asilimia 1.5 huku mwaka 2018 ikiwa 0.6.
"Hakuna jambo jepesi kama kuongeza ujazo wa fedha za msingi ,Benki kuu inaweza kuongeza ujazo wa fedha kwa kununua amana za Serikali "amesema Profesa Lipumba
Profesa Lipumba ambaye ni mchumi pia alieleza kuwa mfumuko wa bei ni mdogo kwa wastani wa asilimia 3 hadi 4 kwa takribani miezi 10 iliyopita hivyo serikali aliishauri serikali kuongeza kasi ya ongezeko la msimu.
Hata hivyo amesema kuwa Baraza kuu limeguswa na yaliyomo katika kitabu cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa uhitaji wa Tume huru ya uchaguzi sambamba na kusononeshwa kwake na kadhia ya mauaji ya Januari 26/27 mwaka 2001.
"Ili kuthibitisha alichikisema katika kitabu chake Baraza kuu linamuomba Mkapa aungane na chama cha CUF ili kuhimiza utekelezwaji wa mapendekezo ya Tume ya Brigedia Jenerali Mbita ikiwemo kuwalipa fidia waathirika wa matukio ya Januari 2001"amesema Profesa Lipumba
Post a Comment