Kampuni Ya Abel & Fernandes Communication, AAR Healthcare yafanya kampeni kuelimisha ugonjwa kisukari
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communication, Fatuma Fernandes akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kituo cha AAR Healthcare Dkt. Akili Msei akizungumza na waandishi wa habari.
Mwandishi wa habari (kushoto) akipimwa ugonjwa kisukari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kituo cha AAR Healthcare Dkt. Akili Msei akizungumza na waandishi wa habari.
Mwandishi wa habari (kushoto) akipimwa ugonjwa kisukari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kampuni ya Abel & Fernandes Communication kwa kushirikiana hospitali ya AAR Healthcare leo imefanya kampeni ya kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa kisukari pamoja na kupima ugonjwa huo bure katika maeneo ya Karikaoo na Tegeta jijini Dar es Salaam.
Kampeni hiyo imelenga kuelimisha umma pamoja na taarifa kuhusu ugonjwa wa kisukari, ambao umeonekana ni hatari kwa afya ya binadamu kutokana takwimu zinaonesha kila sekunde 8 duniani mtu mmoja anafariki, huku hapa nchini kuna watu milioni 4.2 wameathirika na ugonjwa wa kisukari.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya ugonjwa wa kisukari, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abel & Fernands Communication, Fatuma Fernandez, amesema kuwa leo siku ugonjwa wa kisukari duniani, ambapo wameamua kutumia siku hii kuhamasisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari.
"Tunafanya kampeni hii kwa sababu mama yangu anaumwa ugonjwa wa kisukari, hivyo tumeamua kutoa elimu ili watu waujue ugonjwa wa kisukari" amesema Fernandes.
Amesema kuwa ni vizuri kila mmoja akaelewa maana ya ugonjwa wa kisukari ili waweze kujikinga kwa kufanya mazoezi pomoja na kula chakula bora.
Fernandes amefafanua kuwa watu wanaonao kama ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa kawaida kitu ambacho sio kweli kulingana na mazingira husika.
"Kutokana na madhara ya ugonjwa wa kisukari ndiyo maana tunaiambia jamii kisukari inauwa kama magonjwa mengine" amesema Fernandes.
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha AAR Healthcare Dkt. Akili Msei, amesema kuwa kupitia siku hii ya ugonjwa wa kisukari duniania, wataendelea kuonyesha ugonjwa wa kisukari ni hatari.
Amesema kuwa vijana na wazee wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kisukari hapa nchini.
"Leo maeneo ya Tegeta na kariakoo tutakuwa tunapima ugonjwa wa kisukari bure pamoja kutoa ushauri wa kitaalamu" amesema Dkt. Msei.
Mfumo wa maisha ya binadamu imekuwa sababu kubwa ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa haraka zaidi kuliko chochote na hii inatokana na ulaji (vyakula na vinywaji).
Kutokana na uandaaji wa vyakula kutoka vinalimwa hadi kuja kuingia kinywani mwa binadamu imekuwa ni changamoto kwa sababu ya kemikali zinazotumika kutunzia vyakula lakini pia na mtu yeye mwenyewe kama anapenda kula vitu vitamu vitamu ni kirahisi zaidi mtu huyo kuathirika kwa ugonjwa huu.
Uchunguzi uliofanyika huko Marekani unasema kuwa mtu anaependa kula vyakula vyenye sukari nyingi au vitamu kuwa anakiwango kikubwa cha bacteria wabaya mwilini na hao bacteria hupendelea kula vitu vitamu.
Inakuwa ni kirahisi sana kuchochea homone na kushidwa kwa kongosho kubalansi kiwango cha sukari mwilini.
Unene (obesity). Uzito uliopitiza kiwago ni moja ya sababu zinazopelekea mtu kuugua ugonjwa wa kisukari kwa sababu mwili wa mtu mnene unakuwa na sukari nyingi au kuwa na glucose nyingi.
Kurithi. Haijafahamika kuwa nini sababu inayopelekea kurithi huu lakini kama kwenye ukoo kulikuwa na mgonjwa wa kisukari hivyo ugonjwa usishangae mtu kuugua kisukari bila hata ya hizo visababishi vya juu.
Baada ya kujifunza juu ya visababishi vinavyopelekea kuadhirika kwa ugonjwa wa kisukari hivyo ni muhimu kufahamu kuwa mtu anapokuwa na kisukari anakuwa na dalili zipi, zifuatazo ni dalili za mtu alie na ugonjwa wa kisukari.
Post a Comment