Ads

IDRIS SULTAN AMWOMBA RADHI RAIS MAGUFULI.


Na Maria Kaira, Mwambawahabari

Msanii wa vichekesho nchini Tanzania Idris Sultan leo  Novemba 14 amemuamba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kitendo cha kuhariri picha ya Rais na kuiweka katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema alirusha picha hiyo kwa nia njema ya kumtakia kumbukizi ya kuzaliwa Mhe Rais na hakuwa na nia mbaya yoyote tofauti na watu walivyopokea.

 "kutokana na kazi yangu ya vichekesho natakiwa niwe wa tofauti katika kubuni kazi,nachukua nafasi hii kumuomba radhi Rais wangu kwa kilichotokea sikuwa na nia mbaya."amesema


Aidha Mchekeshaji huyo amesisitiza kuwa lengo lake lilikuwa kuhariri picha ya Rais Magufuli ili  kufurahisha watu na kumtaki Kheri ya siku ya kuzaliwa kwake.

No comments