Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ameipongeza TCRA katika Kusogeza huduma kwa Wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuandaa kampeni ya Mnada kwa Mnada kwa kuwa inasaidia sana wananchi kupata huduma kirahisi
Mkuu huyo ameyasema hayo wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa TCRA katika Viwanja vya Gombani Mjini Pemba amesema kwa kusogeza huduma zote muhimu pamoja inawarahisishia wananchi kupata huduma jambo ambalo linamanufaa kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
Hemed amewataka wananchi kutumia vema fursa ya kampeni huyo inapofika katika maeneo yao.
Kampeni ya Mnada kwa Mnada Pemba katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.
Wakazi wa wilaya ya Pemba na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 17 na Zanzibar lengo kuu ni nchi nzima kufikiwa na Kampeni hiyo.
Mkuu wa TCRA Zanzibar Esuphatie Masinga, amesema ni fursa kwa wananchi wa Pemba kufika katika Viwanja vya Gombani kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha kupata usajili wa vitambulisho vya Taifa kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano.
Masung amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.
Mkuu huyo amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.
Masinga amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Hata hivyo amesema kuwa
kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.
TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu wanayoipata katika Kampeni mbalimbali.
Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.
"TCRA tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema.Masinga
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na kupata mwamko wa kutumia simu katika maendeleo.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.
kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Post a Comment