Meya wa Manispaa ya Ilala aipongeza Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa kuchangia damu
Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto ameishukuru na kuipongeza Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa kuendesha Kampeni ya Kuhamasisha Uchangiaji Damu kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Ashura ili kupunguza tatizo la upatikanaji wa damu hospitali.
Aidha, Meya Kumbilamoto ameziomba taasisi na jumuiya nyingine kuiga mfano wa Jumuiya hiyo kwa kujitoa kuchangia damu ili kusaidia wagonjwa wenye mahitaji.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi la uchangiaji damu Meya Kumbilamoto alisema jumuiya hiyo imefanya jambo jema linalotakiwa kuigwa na taasisi nyingine huku akibainisha damu iliyopatikana itapelekwa benki ya damu kusaidia wahitaji.
“ Nitoe shukrani kwa Khoja Shia wamefanya jambo la maana kusaidia kuchangia damu wanaonyesha jinsi gani wanaguswa na maisha ya watu wenye mahitaji ya damu,” alisema Kumbilamoto.
Alisisitiza kuwa uchangiaji damu unaofanywa na jumuiya hiyo unaonyesha kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuliletea taifa maendeleo pamoja na kujitolea bila kujali tofauti za kidini
Kwa upande wake Msimamizi wa uchangiaji damu, Murtaza Chagani alisema jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama kameni hiyo kusaidia upatikanaji damu katika hospitali.
Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kuiunga mkono taasisi hiyo na mpango huo kwa kuchangia damu kusaidia wagonjwa wanaohitaji huku akisisitiza wanatarajia kukusanya unit 350 mpaka 400 mwaka huu.
Naye Afisa Uhamasishaji wa Mpango huo- Kanda ya Mashariki, Fatma Mjungu alisema tangu mwaka 2005 wanafanya kazi na jumuiya hiyo na kwamba wanatarajia kkukusanya chupa 600 za damu.
Alifafanua kuwa mwaka huu watakusanya chupa 375000 za damu na kuyaomba madhehebu mengine kufanya uchangija damu kusaidia wagonjwa.
Siku ya Ashura ni siku mahasusi ya kuomboleza kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) aliyeuawa kikatili huko mji wa Kerbala nchini Iraq na Jeshi la Yazid.
Post a Comment