Viongozi wa Dini Mbalimbali nchini wawasisitiza wanawake kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Hussein Ndubikile, Mwambawahabari
Kamati ya Viongozi wa Dini Mbalimbali nchini,imewataka wakinamama kuwa na uthubutu wa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa lengo la kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es salaam katika Kilele cha Kongamano kuhusu Nafasi ya Mwanamke katika Uongozi wa kuchaguliwa na Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Charles Kitima ambapo alisema wanawake wanatakiwa wawe na uthubutu kuchukua fomu na kugombea nafasi katika uchaguzi huo.
Padri Kitima alisema kabla ya kongamano hilokulitanguliwa na Semina ya iliyofanyika katika ofisi za baraza hilo iliyolenga kuwajengea uwezo wanawake kujitokeza kugombania nafasi mbalimbali za uongozi.
"Mafunzo haya yamewawezesha akinamama kutambua wajibu wao katika kujitokeza kushiriki kugombea nafasi kwenye chaguzi mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa serikali ya mitaa pamoja na uchaguzi mkuu," alisema Kitima
Kitima alisisitiza kuwa viongozi wa dini wamejitoa kuheshimu mitazamo ya wakinamama kwenye kupambana na changamoto mbalimbali za kimazingira japokuwa dini hazina vyama wameona kuwa wanawake wakipewa nafasi huzitumia vizuri.
Alifafanua kuwa wanaume wanatakiwa kuwatia moyo wanawake wajitokezee kwa wingi kuchukua fomu na kugombea nafasi za uongozi na kwamba itasaidia kuiletea nchi maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa taifa Waislam Wanawake kutoka Bakwata Hajat Shamimu Khan alisema wanamke ni nguzo kubwa katika familia na taifa kwa ujumla hivyo ni muhimu kuwa na uthubutu kuwania nafasi za uongozi .
"Mafunzo yalikuwa mazuri sana yametujenga akinamama kuweza kukabiliana na ushindani mkubwa wa kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali ya mitaa," alisema Khan.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Mennonite Dayosisi ya Mashariki Maira Migire amewataka wanawake kuepuka baadhi ya misemo inayowakatisha tamaa badala yake wachangamkie fursa za kuwa viongozi katika jamii inayowazunguka.
Askofu Mkuu wa Katoliki Jimbo la Bukoba Mjini Method Kilaini amewasihi wanawake kuwania nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya kata hadi taifa na kuwasisitiza wakinababa kutowavunja moyo.
Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) Renatha Selemani alisema matamko ya Shirika la Haki za Binadamu yanatambua usawa kati ya wanawake na wanaume katika nafasi za uongozi na kusisitiza Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa haki mwanamke kushiriki katika nafasi za uongo

Post a Comment