DC MJEMA ATOA AGIZO KWA WAMILIKI WA NYUMBA WANAOIFADHI WAHAMIAJI HARAMU ILALA KUPEWA KIBANO
Mwambawahabari
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ,amewataka wamiliki wa nyumba wilayani Ilala kuwafichua wahamiaji haramu ndani ya nyumba zao watakao kaidi nyumba kuchukuliwa na serikali
Mjema alitoa agizo hilo Wilayani Ilala leo wakati wa kuzindua mkakati wa udhibiti wahamiaji haramu Wilayani humo kwa Watendaji kata na Maofisa Tarafa .
"Tunanza oparesheni nyumba kwa nyumba katika wilaya yangu wale wamiliki wa nyumba ambao wanawaficha katika nyumba zao nawaomba wawafichue mara moja hatua kali zitachukuliwa ikiwemo nyumba zao kutaifishwa na Serikali kwa kujihushisha na biashara ya kuifadhi raia wa kigeni wakijua ni kosa kisheria"alisema Mjema.
Mjema alisema ukikamatwa unaifadhi wahamiaji haramu mali zako zote zitachukuliwa ikiwemo magari.
Alisema mhamiaji haramu ni mgeni yeyote wa nchi nyingine anayeingia nchini bila kufuata taratibu kwa ofisa uhamiaji mpakani au ni raia wa kigeni ambaye ameingia nchini na muda wa kuishi nchini aliyopewa kuwepo tayari umekwisha bila kufuata taratibu .
Aidha alisema madhara ya kuifadhi wahamiaji haramu ni kuhatarisha amani ya nchini na Ilala kwa ujumla..
Alitaja madhara mengine ya kukumbatia wahamiaji haramu migogoro katika ardhi,rasilimali za wazawa kuwanufaisha wahamiaji haramu mfano elimu,mashamba,ajira,biashara na mikopo ya Benki .
Pia kusababisha migogoro kwa kutokuwa na wazalendo kujipenyeza katika nchi kupata vitamburisho vya Taifa,vya kura vyeti vya kuzaliwa ili waweze kuhalalisha ukaazi wao hatimaye kuomba uongozi.
Amewataka Maofisa Watendaji wa Kata na maofisa Tarafa kusimamia misingi ya kazi yao kwa weledi kwa kuheshimu mipaka yao na kufatilia Daftari la mkazi kila mgeni ambaye anaingia eneo la kata .
Kwa upande wake Naibu Kamishina wa Uhamiaji DCI Pili Zuberi alisema wahamiaji haramu wamekuwa na tatizo kubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Ilala na amekuwa akikumbana na changamoto jinsi ya kupambana nalo.
Kamishina Pili alisema moja ya changamoto ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo kutokuwepo kwa taratibu wa viongozi wa mitaa na kata kuwatambua raia wa kigeni wanaoingia katika maeneo yao ikiwemo kufahamu dhumuni la ujio wao.
Alisema baada kubaini tatizo ili la la kuwepo na kuongezeka kwa hamiaji haramu ofisi ya uhamiaji mkoa imeandaa mkakati wa kupambana nao na kudhibiti hali hii kwa kuweka mkakati na kuzindua kwa kuwashirikisha watendaji na maofisa tarafa.
Mwisho
Post a Comment