TMA yatangaza mvua za Vuli, kuanza Oktoba mwaka huu
Mamlaka mbalimbali zimetakiwa kuandaa mikakati ya kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za vuli zinazotarajia kuanza mwezi oktoba hadi desemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijiji Dar es Salaam Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes kijazi, amesema kuwa kuelekea katika mvua za vuli ni vizuri mamejimenti husika wakachukua hatua.
Amesema kuwa katika mvua za vuli maeneo yanayozunguka ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) yanatarajia kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Amesema maeneo ya Pwani ya kaskazini pamoja na nyanda za juu kaskazini mashariki kunatarajia kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani.
''Ukanda wa ziwa viktoria mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi oktoba mwaka huu" amesema Dkt. Kijazi.
Dkt. Kijazi ameeleza kuwa kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na pwani ya kaskazini, huku maeneo ya kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Amefafanua kuwa mvua za vuli ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini -mashariki, pwani ya kaskazini pamoja na visiwa vya unguja na pemba, ukanda wa ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa kigoma.
Post a Comment