Ads

TAMASHA LA KUDUMISHA TAMADUNI AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA TANZANIA.

Maandalizi ya tamasha kubwa la kudumisha tamaduni Afrika Mashariki  maarufu kama JAMAFEST ni wazi Sasa yamekamilika ambapo nchi wanachama za jumuiya ya (EAC) huku Tanzania ambayo ni mwenyeji wa tamasha Hilo kwa mwaka huu ikitakiwa kuendelea kudumisha tamaduni ili kunogesha tamasha Hilo sanjari na kukuza utalii.
Akizungumza na wanahabari mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao Cha maandalizi ya tamasha Hilo la nne la sanaa na utamaduni Afrika Mashariki (JAMAFEST)2019  Katibu  Mkuu Wizara ya  Habari, Sanaa , Utamaduni na Michezo Bi. Susan Mlawi amesema kuwa  litakayofanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam
Bi Mlawi ameongeza kuwaTamasha hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa lengo la kukuza sekta ya utalii nchini lakini pia kukuza lugha ya kiswahili katika nchi mbalimbali duniani ambayo imezidi kukua kwa kssi siku Hadi siku
Aidha Tamasha hilo litatoa fursa mbalimbali kwa wafanya biashara kuonyesha bidhaa zao ili kukuza uchumi wao na kuongeza kuwa  litatoa hamasa kwa watanzania kuweka kipaombele katika utamaduni wao pasi na kuendeleza tamaduni za kigeni ambazo kwa sehemu zinaathiri Utamaduni za kiafrika.
"aTamashahli litahusisha zaidi ya nchi sita(6) za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda, Burundi na Sudani ya kusini"alisema Bi Mlawi
Kwa upande wake  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Taifa, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fisoo Alisema kwenye Tamasha hilo kutakuwepo na maonyesho mbali mbali ikiwemo mafunzo kwa wadau mbalimli, Ngoma za asili, Sanaa na michezo na filamu mbalimbali.
Hivyo amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utajiri uliopo Afrika."Hakika tamasha hili kwa mwaka huu litakuwa la kuvutia sana hivyo niwaombe watanzania wajitokeze kwa  wingi kushiriki"alisema Bi Joyce Fisoo.             
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Suzani Mlawi akifungua kikao cha  maandalizi ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki 2019 (JAMAFEST) litakalofanyika nchini Tanzania  mwezi septemba kutoka kulia ni Bakaye Lubega Ofisa Utamadunina Michezo Jumuiya ya Afrika Mashariki na katikati ni Nyakana Oswald  kutoka  Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Suzani Mlawi akifafanua jambo wakati akifungua kikao cha  maandalizi ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki2019 (JAMAFEST) litakalofanyika nchini Tanzania  mwezi septemba kutoka kulia ni Bakaye Lubega Ofisa Utamadunina Michezo Jumuiya ya Afrika Mashariki na katikati ni Nyakana Oswald  kutoka  Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda, Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa JNCC jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Taiga, Joyce Fisoo  kutoka Bodi ya Filamu Tanzania akifurahia jambo wakati wa kikao hicho cha maandalizi

No comments