CUF YAJIANDAA KUFANYA MKUTANO MKUU TAIFA.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Chama Cha Wananchi (CUF) kinatarajia kufanya mkutano mkuu Taifa kwa ajili kufanya maboresho na mabadiliko mbalimbali ya viongozi pamoja katiba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam, Kaimu katibu mkuu Chama Cha Wananchi Taifa (CUF) Jafar Mnek, amesema kuwa mkutano mkuu unatarajia kufanyika march I4 hadi I5 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kabla ya mkutano mkuu kutakuwa na vikao vya wajumbe wa baraza kuu pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu taifa.
"Kupitia mkutano huo utafanya uchaguzi wa viongozi taifa, kufanya mabadiliko ya katiba ya chama, nawaomba wajumbe wa mkutano wajitokeze kwa wingi" amesema Kaimu katibu mkuu.
Ameeleza kuwa kupitia mkutano huo watapata fursa ya kufanya mabadiliko katiba ya chama ili kuendana na katiba ya vyama vya siasa ambavyo tayari imeanza kufanya kazi.
Post a Comment