BOOMPLAY INASHEHEREKEA Na WANAMUZIKI WA KIKE KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Boomplay ni app nambari moja kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, inasherehekea Siku Ya Wanawake Duniani 2019 ikiwa na kampeni mpya ya “Boom Queens”.
Vanessa Mdee, Rihanna,
Tiwa Savage, Fena Gitu na wengine wengi, ni miongoni mwa wanawake wenye
vipaji ambao wameendelea kubadilisha tasnia ya muziki duniani.
App ya Boomplay
itakuwa na muonekano wa tofauti hasa katika Siku Ya Wanawake duniani tarehe 8
Machi, lengo likiwa ni kuonesha na kukuza kazi za wanawake katika muziki.
App
itapambwa na nyimbo, albamu pamoja na playlist za wanawake katika vipengele
vyote kwenye ukurasa wa kwanza.
Boomplay pia itakuwa
na kampeni kabambe ambayo itatoa fursa ya kukuza mauzo ya kazi za wanawake
ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist ya BOOM QUEENS.
Playlist hiyo
itakuwa na nyimbo za wasanii bora wa kike tu.
Katika kampeni hii,
Meneja Mahusiano wa kampuni ya Boomplay, Bi Tosin Sorinola amesema, “majadiliano
juu ya usawa wa kijinsia ni moja ya mambo ambayo ni muhimu kwetu kama jukwaa lenye nia kubwa ya kukuza wanawake katika
muziki, katika njia njema kadri iwezekanavyo. Kampeni hii sio kwa mara moja tu,
ni endelevu, na hili litadhihirishwa katika shughuli zetu za kila siku”.
Katika mwezi huu wa
kuadhimisha Siku Ya Wanawake Duniani, watumiaji wa Boomplay kupitia simu zao za
Android na iOS watapata fursa ya kujishindia simu mpya ya iPhone XS na zawadi
nyingine kem kem nchini Tanzania,
Kenya, Nigeria na Ghana.
Ili
kuonesha upendo kwa wasanii wa kike katika tasnia ya muziki, basi jishindie
zawadi hizi kwa ku-subscribe kwenye app ya Boomplay kwenye vifurushi
vinavyopatikana (vya siku, wiki na mwezi) na pia sikiliza playlist ya Boom
Queens.
App ya Boomplay ambayo
ina watumiaji zaidi ya milioni 42 dunia kote, hivi karibuni ilizindua app hiyo
kwenye jukwaa la iOS. Hakika Boomplay inajivunia kuwa na nyimbo na video zaidi
ya milioni 5 kutoka kwa wasanii wa Tanzania na wakimataifa.
Post a Comment