BENKI YA KCB YAKUTANA NA WADAU KUTAFUTA MAENDELEO.
Bw. Ernest Jackinda, Afisa Masoko wa TANAPA akiongea na wageni waalikwa katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za
Kuendelea.
Bw. Masika Mukule, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Masuala ya Kibenki akiongea na wageni waalikwa wakati wa maongezi ya ana kwa ana katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.Picha No
Bi Christine Manyeye,Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusaino akijibu maswali kutoka kwa wafanya biashara wa jijini Arusha katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Na Mwandishi Wetu.
Benki ya KCB Tanzania imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Benki ya KCB Tanzania imefanya kongamano la kwanza la Biashara Club kwa mwaka 2019 jijini Arusha baada ya kuandaa kongamano kama hilo jijini Mwanza mwishoni kwa mwaka 2018.
Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara nje na ndani ya nchi.
Tangu kuzinduliwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira
yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki
kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha
mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.
Biashara Club jijini Arusha lilifanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019
na lilikuwa na lengo mahususi la kukutanisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii wakiwemo wafanyabiashara.
Kongamano hilo lilifanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yakwanza ilikuwa mahusu kwa wateja wa benki ya KCB.
wapatao 250, huku sehemu ya pili ikiwa ni jukwaa la wazi kwa wakazi wengine wa
Arusha kupata elimu ya huduma za kibenki kutoka kwa wataalam wa Benki ya KCB.
Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bi. Christine Manyenye alisema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kama Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania
Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Kwa upande wake Meneja wa Tawi, KCB Bank Arusha, Bi. Judith Lubuva
aliwapongeza wafanya biashara, wadau na wakazi wa Arusha kwa kuhudhuria
kongamano. Aliongeza kwamba kongamano hilo limefanyika kwa wakati muafaka ambapo sekta ya utalii inaendelea kuimarika katika kanda ya kaskazini na Tanzania kwa ujumla.
Naye Abdul Juma, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME) aligusia fursa tofauti zinazoletwa na Biashara Club zikiwemo kuwakutanisha wafanyabiashara mbali mbali wa nje na ndani ya nchi, kupanua wigo wa masoko kupitia safari za pamoja kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini.
Juma aliwahakikishia wadau kwamba KCB Bank ina dhamira ya kuinua sekta ya
utalii kwa kuitambulisha Tour Operator Account inayowezesha malipo ya
kieletroniki pamoja na kuwana faida zingine zikiwemo huduma kwa njia ya
mtandao kuwa bure na kutoa pesa bure.
Akiongea katika warsha hiyo, mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Mr.
Ombeni Urio aliyekuwa mshauri wa masuala ya kodi, alisisitiza umuhimu wa
wafanya biashara hao kufuata kanuni za kodi. Aliipongeza Benki ya KCB kwa
kumualika ili aweze kutoa elimu hiyo ambayo ilikuwa inahitajika kwa sana.
Benki ya KCB inatajwa kuwa ni kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka
1896 kisiwani Zanzibar.
Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi 6 za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia.
Leo hii inamtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.
Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda
na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital
na KCB Foundation.
Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na tok hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini.
Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
Post a Comment