STERLING AJITOA TIMU YA TAIFA.
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester City Raheem Sterling amejitoa katika kikosi cha England katika mechi dhidi ya Uhispania na Uswizi.
Mchezaji huyo wa miaka 23 anaumwa mgongo shirikisho la soka limesema.
Sterling ndiye mchezaji pekee aliyekosekana wakati timu hiyo ilipoteremka dimbani St George Jumatatu.
Hakuna mchezaji aliyepangwa kuichukua nafasi yake, hatua inayomuacha meneja Gareth Southgate akiwana kikosi cha wachezaji 22 kwa mchuano wa ligi ya kitaifa ya UEFA dhidi ya Uhispania na Jumanne katika mchuano wa kirafiki na Uswizi.
Kikosi kipya cha England:
Makipa: Jack Butland (Stoke), Jordan Pickford (Everton), Alex McCarthy (Southampton)
Walinzi: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Fabian Delph (Manchester City), Joe Gomez (Liverpool), Harry Maguire (Leicester City) Danny Rose (Tottenham Hotspur), Luke Shaw (Manchester United), John Stones (Manchester City), James Tarkowski (Burnley), Kieran Trippier (Tottenham Hotspur), Kyle Walker (Manchester City)
Wachezaji kiungo cha kati: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Manchester United), Ruben Loftus-Cheek (Chelsea)
Wachezaji kiungo cha mbele: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Marcus Rashford (Manchester United), Danny Welbeck (Arsenal)
Post a Comment