BAKI SIMBA AFANYA MAKUBWA.
Beki wa klabu ya Simba, Pascal Wawa, ameahidi kuendelea kujifua zaidi ili kuepuka ushindani wa namba kutona na timu yake kuwa na kikosi kipana, imeelezwa.
Wawa ambaye aliwahi kuichezea Azam FC, amesema ataendelea kujifua zaidi kwa nguvu zote ili kuhakikisha hachuji jambo ambalo litamuwezesha kuimudu vema nafasi yake.
Wawa ambaye ni beki wa kati amesema kujituma kwake mazoezini kutampa nguvu na morali ya kuzidi kufanya vema zaidi ili kuonesha kuwa hajasaliwa Simba kupoteza muda.
Wawa alianza kufanyiwa majaribio na Simba kwenye mashindano ya Kagame yaliyofanyika hapa nchini hivi karibuni na baadaye kupewa mkataba wa mwaka mmoja na mabosi wake.
Beki huyo alisaini mkataba huo baada ya kuwashawishi kutokana na kiwango alichoonesha na sasa amekuwa mchezaji tegemeo ndani ya kikosi.
Post a Comment