Ads

Christopher Chiza aapishwa bungeni


Image result for picha za christopher chiza

Mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeanza rasmi leo tarehe 4 Septemba, 2018 ambapo ilikuwa kikao cha kwanza na kuongozwa na Spika Job Ndugai.
Katika kikao hicho, Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza aliyechaguliwa kwenye uchaguzi mdogo wa tarehe 12 Agosti, 2018 alikula kiapo cha uaminifu mbele ya bunge.
Akiapa mbele ya Bunge, Mhandisi Chiza aliapa kuitumikia, kuilinda na kuitetea katiba ya nchi kwa moyo wake wote.
Mhandisi Chiza alishinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema, marehemu Kasuku Bilago kufariki dunia. Katika uchaguzi huo alichuana vikali na mgombea wa Chadema, Elia Michael.  

No comments