MODRIC ANYAKUA TUZO MCHEZAJI BORA ULAYA.
Kiungo wa Klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Croatia, Luka Modric amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya akiwafunika Mo Salah wa Liverpool na Cristiano Ronaldo wa Juventus.
Kipa wa Real Madris, Kyle Navas, ametwaa tuzo ya goli kipa bora wa michuano ya Uefa msimu wa mwaka 2017/18.
Beki kisiki wa Real Madrid, Sergio Ramos, ametwaa tuzo ya beki bora kwenye michuano ya Uefa msimu wa mwaka 2017/18.
Aidha, Cristiano Ronaldo aliyekuwa Real Madrid kabla ya kutimkia Juventus, ametwaa tuzo ya mshambuliaji bora wa michuano ya Uefa msimu wa mwaka 2017/18.
Pia, Legendari, David Bechkam amepewa tuzo ya heshima kutoka uefa kutokana na mchango wake mkubwa katika soka.
Walioshika nafasi kuanzia ya 4 za mchezaji bora ni;
4 Antoine Griezmann (Atlético & France) – 72 alama
5 Lionel Messi (Barcelona & Argentina) – 55 alama
6 Kylian Mbappé (Paris & France) – 43 alama
7 Kevin De Bruyne (Manchester City & Belgium) – 28 alama
8 Raphaël Varane (Real Madrid & France) – 23 alama
9 Eden Hazard (Chelsea & Belgium) – 15 alama
10 Sergio Ramos (Real Madrid & Spain) – 12 alama
Post a Comment