Ads

SIMBA KUKUTANA NA TFF KUJADILI SAKATA LA WACHEZAJI SITA


Shirikisho la Soka nchini (TFF) leo linakutana na uongozi wa klabu ya Simba kunako makao makuu yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam.

TFF wanakutana na Simba kwa lengo la kuweza wazi sakata la kuondolewa kwa wachezaji wake 6 ambao walikuwa wameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Uongozi wa shirikisho hilo utaweza wazi juu ya suala hilo sambamba na Simba wenyejewe juu ya wachezaji hao ambao wamekuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari.

Wachezaji wa Simba waliondolewa kwenye kikosi na Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike kwa kuchelewa kuripoti kambini huku Kipa Aishi Manula pekee akiwahi.

Wachezaji ambao waliondolewa ni Shiza Kichuya, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco na Erasto Nyoni.

Idaidi ya wachezaji walipaswa kuanza mazoezi na wenzao jana kwenye Uwanja wa Bocco Veterani tayari kujiandaa na mchezo wakufuzu kuelekea AFCON dhidi ya Uganda, Septemba 8 2018 huko Kampala.

No comments