Naibu Waziri Mhe.Shonza atoa wito kwa Wasanii Nchini kuhamasisha Utalii wa Ndani.
Mwambawahabari
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Utalii Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara Bibi. Eva Mallya (kulia) baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ikiwa ni hatua ya kuhamasisha utalii wa ndani chini ya uratibu wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akingalia ramani inayonyesha
vivutio mbalimbali pamoja na wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya
Taifa ya Ziwa Manyara jana Jijini Arusha wakati wa ziara ya kutembele
hifadhi hiyo, wengine ni Rais wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network
(TAGOANE) Dkt. Godwin Maimu (katikati) na kulia ni Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akipokea cover ya tairi la gari
lenye nembo ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara kutoka kwa Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga .
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akisikiliza maelekezo kutoka
kwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga
kuhusu chemchem ya maji moto ambayo inapatikana katika hifadhi
hiyo alipofanya ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wasanii na
watanzania kwa ujumla lengo ni kuwa na utamaduni wa kutembelea
vivutio hivyo .
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiangalia uoto wa asili ambao
hupatikana katika Hifadhi ya Taifa ya ya Ziwa Manyara wakati wa ziara
ya kutembelea hifadhi hiyo hapo jana Jijini Arusha chini ya uratibu
wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE).
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiwashukuru wasanii na wajasiriamali
kutoka Jiji la Arusha ambao aliambatana nao katika ziara ya kuhamasisha
utalii wa ndani, iliyoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artist
Network (TAGOANE) lengo ikiwa ni kuwajengea watanzania utamaduni wa
kupenda kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kukuza uchumi
wa nchi. ( Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha)
Post a Comment