ASALI YA TANZANIA NIBORA IMEPATA TUZO MAREKANI
Mwamba wa habari
Na. John Luhende
Watanzania wameshauriwa kutumia asali inayozalishwa na wafugaji nyuki wa ndani kwakuwa ni asali bora kuliko zingine.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Follow the Honey Tanzania Kaizirege Kamara, Katika maonyesho ya 42 Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa Dar es Salaam na kusema kuwa Asali inayozalishwa Tanzania imepata soko kubwa Ulimwenguni kutokana na ubora wake.
"Asali hii unayoiona tunauza Marekani na imepatatuzo sasa
minashangaa kuona mtu a naenda kununua Asali Arabiani wakati hatanyuki
hawafugi ,"amesema
Aidha amesema wanahamsisha wananchi kutumia Asali ya
Tanzania sikwa sababu kuwa ni Tanzania bali ni kwa sababu ni bora kwa
Afya.
Ameongeza kuwa walianzisha kilimo nyuki pia kwa sababu ya
kutunza mazingira na kuanza kutengeneza bidhaa mbali mbali za
viwandani.
Pamoja na hayo amesema sektayanyuki ni mtambuka nainasaidia na inasaidia kukuza uchumi wa viwanda na uchumi wa mwananchi.
Post a Comment