TTCL MFANO WA KUIGWA NA MASHIRIKA
Kutokana
na faida waliyoipata mwaka 2017 hadi kutoa gawio la Sh1.5 bilioni kwa
Serikali, Rais John Magufuli amesema wafanyakazi wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL) wana haki ya kuongezewa mishahara.
Akizungumza
leo Juni 21 wakati wa hafla ya Serikali kupokea gawio hilo kutoka TTCL,
Rais amesema hata kama hajapandisha mishahara kwa watumishi wote wa
Serikali lakini shirika hilo limeonyesha jinsi linavyotanguliza masilahi
ya Taifa mbele.
“Tangu
shirika hili lianzishwe mwaka 1993 halijawahi kutoa gawio. Uchapakazi
wenu unaonekana. Ingawa sijaongeza mishahara kwa watumishi lakini ninyi
ayayaya,” amesema Magufuli.
Serikali
imepokea gawio kutoka shirika hilo ukiwa ni mwaka mmoja tangu
lilipobadilishwa kutoka kuwa kampuni na kuanza kujiendesha kwa faida.
Rais ameyataka mashirika ya umma kujiendesha kwa faida na kutoa gawio huku akiyasisitiza kujiendesha kwa ufanisi.
Amesema mwaka 2005 kulikuwa na mashirika 92, lakini ni manne yaliyotoa gawio la Sh130.868 bilioni.
Baadaye
yaliongezeka mashirika 24 yaliyotoa gawio la Sh149.3 bilioni mwaka 2006
na mwaka 2007 mashirika 38 yaliipa Serikali Sh677 bilioni.
Post a Comment