SIMBA YAREJEA KAMBINI KUANZA KUJIWINDA NA KAGAME
Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi leo ya kujiandaa na michuano ya KAGAME inayotarajiwa kuanza jijini Dar es Salaam Juni 28 2018.
Mazoezi hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa White Sand uliopo uliopo jijini Dar es Salaam.
Simba
wameanza mazoezi ya kwanza baada ya mapumziko mafupi ambayo walipewa
kumalizika na sasa wamerejea tena kambini kuanza kujiwinda na mashindano
hayo ya CRCAFA.
Kuelekea
michuano ya KAGAME, inaelezwa baadhi ya nyota wa kikosi hicho ambacho
ni bingwa wa msimu huu katika ligi watakosekana ili kuwapa mapumziko.
Jonas Mkude na Haruna Niyonzima ni baadhi ya wachezaji walioripotiwa kukosekana kwenye mashindano hayo.
Post a Comment