Manispaa ya Ilala yafungia maabara bubu
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
MANISPAA ya Ilala imezifungia mahabara bubu na maduka ya dawa yasio na sifa ambayo yanatoa huduma kinyume cha sheria.
Oparesheni hiyo endelevu ya kuzifungia mahabara hizo na maduka ya dawa imeanza Dar es Salaam jana katika Jimbo la SEGEREA, UKONGA na Ilala.
Akizungumza katika ziara Mratibu wa Vituo Binafsi Manispaa ya Ilala Dkt. Wille Sangu alisema maduka ya dawa ambayo wanayafungia ambayo wahudumu wake hawana sifa za kuendesha huduma hiyo na wengine wanatoa huduma za kuwachoma sindano wateja tofauti na kibali chao.
"Ofisi ya Mganga Mkuu Ilala imeweka utaratibu wake kila mwaka kufanya ziara ya ukaguzi wa kuzikagua mahabara bubu ambazo hazina vibari na Duka za dawa Mara baaada kuwakamata kuwataka wafuate taratibu za usajili ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala" alisema DKT Sangu
Sangu alisema katika oparesheni hiyo pia walifunga maduka ya dawa ambayo yalikuta watoa huduma wasio na sifa na maduka mengine yakijiusisha na upimaji VVu,utoaji mimba na uchomaji sindano.
Aliwataka watoa huduma wote ambao wamekamatwa jana kwenda Manispaa ya Ilala kwa ajili ya taratibu .
Amewataka Wananchi watumie vituo vya tiba Kwa ajili ya matibabu mahabara kwa ajili ya vipimo na maduka ya dawa kwa ajili ya kununua dawa, ukikuta duka la dawa linatoa tiba au mahabara wanatoa tiba ni hatari kwa AFYA yako.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa MANISPAA ya Ilala Dkt. Emily Lihawa aliwataka Wamiliki wa vituo vya kutolea huduma katika wilaya hiyo, wafuate miongozo yote ya hutoaji huduma ya Afya.
Dkt .Lihawa aliwataka Wamiliki watoe huduma kulingana na vibali vyao wasikiuke kanuni,kikubwa wafuate miongozo ya kukinga na kuthibiti maambukizi wakati wa utoaji huduma za afya.
Katika ziara hiyo ilifungia mahabara Bubu na Zahanati KIWALANI, TABATA, KIVULE ,Minazi mirefu na kuwataka Wamikiki wote kufuata taratibu za usajili.
Post a Comment