Ads

YANGA NA AZAM JUMAMOSI ,CHAMANZI MOTO UTAWAKA


Kwa mara ya kwanza, Yanga itacheza mechi yake ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chanazi jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii saa moja usiku.

Yanga watakuwa wageni wa Azam FC na mechi hiyo imepitishwa kuchezwa usiku ikiwa ni ya kwanza ya Yanga katika uwanja huo.

Kawaida mechi kubwa kama hiyo ya Azam dhidi ya Yanga huchezwa kwenye Uwanja wa Taifa au Uhuru.

Simba ndiyo walikuwa wakwanza msimu huu kuwa timu kubwa kucheza mechi ya ligi Chamazi katika mechi iliyoisha kwa sare.

No comments